JKT RUVU WILDLIFE KUMLETA MFALME WA NYIKA SIMBA-MEJA KUWASSA

Meja Seif Hassan Kuwassa  wa Kikosi Cha JKT Ruvu 832,Kilichopo Mlandizi Mkoani Pwani pichani juu akifurahia na Pundamilia.kwenye bustani hiyo.

Uongozi wa Bustani ya wanyamapori ya JKT Ruvu 832 iliyopo Mlandizi Kibaha Mkoani Pwani umejipanga kumleta  mfalme wa nyika Simba ikiwa ni katika kuiongezea hadhi bustani hiyo.

Akizungumza  katika mkutano na Waandishi wa Habari hivi karibuni  katika mkutano uliofanyika kwenye bustani hiyo  Meja  Seif Hassan Kuwassa amesema  kuwa bustani hiyo yenye ukubwa wa heka 70 imezinduliwa mwezi Mei mwaka huu huku ikiwa  imejengewa uzio yenye wanayamapori aina saba kwa sasa lakini hivi karibuni  tumejipanga kumleta Simba ambaye atafugwa kwenye banda maalumu tofauti  na ilivyo kwa wanyamapori  waliopo hivi sasa ambao wamekua wakitembea kwa uhuru kama mnavyoona amesema Meja Kuwassa. 
Aidha Meja Kuwassa ametaja  aina ya wanyamapori  wanaopatikana hivi sasa kwenye bustani   hiyo ya 'Ruvu Wildlife' kuwa ni Twiga, Pofu,Pundamilia,Swala aina mbili Impala na Pongo,Nyumbu na ndege wa aina mbili Mbuni asiyeruka na Korongo.

Amesema kuwa wanyama hao ambao ukifika wanaonekana wakiwa wanatembea bila kizuizi chochote wamepatiwa mafunzo  ya kuishi na binadamu hivyo hawana madhara.

"Kabla ya kuachiwa kweye bustani wanyamapori  hawa wamepatiwa mafunzo na mtaalamu wa wanyamapori  ndiyo maana wanaishi kiraafiki hata wakiona watu wanawafuata bila ya uoga wa aina yeyote, mtalii  akifika kuna maelekezo atapatiwa na wataalamu wetu  hivyo atakuwa huru kuwalisha chakula maalumu  na kupiga nao picha kwa karibu" amesema Meja Kuwassa. 

Meja Kuwassa  amezungumza  kwa niaba ya Mkuu wa Kikosi Cha JKT Ruvu 832  Kanali Peter Elius Mnyani, ambaye ndiye aliyetoa wazo la kuanzishwa kwa mradi huo ameongeza kwa kusema kuwa kuna wanyama wengine ambao wanapatiwa mafunzo na baada ya miezi sita watawaachia kwenye bustani hivyo idadi ya wanyama hao itaongezeka na kuleta kivutio zaidi.

"Wazo la kuanzishwa kwa bustani hii limetoka kwa Kanali Mnyani  akalifikisha kwenye  bodi likapita bila kupingwa na kuzinduliwa mwezi Mei 2024 " amesema  Meja Kuwassa. 

"Mradi  huu una lengo la kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan jinsi anavyoitangaza nchi  kwa kupitia utalii ndani na nje ya nchi  hivyo nasi tumeamua kuutangaza utalii wa ndani amesisitiza Meja Kuwassa. 
Baadhi ya wanyamapori  wakijivinjari kwenye bustani ya 'Ruvu JKT Wildlife' iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani

Meja Kuwassa amesema  kuwa tangu bustani ilipozinduliwa muitikio  wake unaridhisha kwani hupata watalii wa nje  saba ndani ya juma na mwishoni mwa wiki familia mbalimbali  huenda kubarizi katika bustani  hiyo. 

Amesema kuwa huduma zingine zinazopatikana ni pamoja na kuwa na mabwawa ya kuogelea kwa wakubwa na watoto, kadhalika  kuna michezo mbalimbali  ya watoto kama kuendesha gari ,baiskeli inapatikana,
chakula kinapatikana pamoja  na 
vinywaji aina zote.

Meja Kuwassa  ametoa wito kwa wakaazi wa maeneo ya Mlandizi  na viunga vya jirani ndani na nje ya Mkoa wa Pwani  ambao hawajawahi kwenda mbugani kuona wanyamapori wanakaribishwa 'Ruvu Wildlife' wakajionee wanyama kwa uhalisia kwa sababu  panafikika kwa urahisi ni mkabala na barabara  ya Morogoro  na kuna mandhari nzuri kwa ujumla. 

"Huu mradi unajitegemea  na tumefuata taratibu zote zinazohusu Wanyamapori" amesema Meja Kuwassa. 
Baadhi ya wanyamapori  akiwamo Twiga wakijivinjari kwenye bustani ya 'Ruvu JKT Wildlife' iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani

Meja Seif Hassan Kuwassa  wa Kikosi Cha JKT Ruvu 832,Kilichopo Mlandizi Mkoani Pwani akifafanua jambo kwenye Mkutano na  na Waandishi wa Habari  hawapo pichanai   kwenye mkutano uliofanyika kwenye  bustani  hiyo .

Kutoka kushoto ni Meja Seif Hassan  Kuwassa  na Mtaalamu wa wanyamapori wa 'Ruvu Wildlife 'Ezekiel Mollel wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.

Pichani ni Mtaalamu wa wanyamapori  na.mkufunzi wao Ezekiel Mollel. 
Kutoka kushoto ni Meja Seif Hassan  Kuwassa  akiwa na Mtaalamu wa wanyamapori wa 'Ruvu Wildlife 'Ezekiel Mollel wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.

Mtaalamu na Mkufunzi wa Wanayapori Ezekiel Mollel amesema  kuwa kuna faida ya kwenda mbugani ama bustani ya wanyamapori  unaondoa sonona na kuleta afya ya  akili.

"Binafsi nina utaalamu wa kongea na wanyama hivyo wakifika hapa wanafungiwa  na kupatiwa mafunzo ndani ya miezi sita ndipo wanaachiwa  huru kwrnye bustani  kama mnavyoona hawana madhara kwa binadamu,wakiona watu wanawafuata kama wanawakaribisha mazingira ya hapa Ruvu ni rafiki kwao wanajiona kama wako mbugani pana rutuba majani yanamea wanakula na hivi vyakula tunavyowapa ni maalumu nikama vitafunywa mbavyo ndivyo watalii wakija tunawapa wawalishe haturuhusu mtu kuingia  na chakula au kumpa mnyama kitu chochote cha tofauti" amesema Mollel. 

"Kiingilio  ni 50,000 kwa mkubwa mtoto 30,000  pia tunazo bei za wanafunzi wa vyuo pia tunaruhusu watu kuja kusherehekea  siku zao za kuzaliwa na Pre Wedding.

Post a Comment

0 Comments