Umoja wa Wafanyabiashara wa Mtaa wa Mahiwa na Zigua Kariakoo Jijini Dar es Salaam wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati operesheni ya kuondoa wafanyabiashara wa kanzu, Mitandio pamoja na vitu mbalimbali vya maharusi wa dini Kiislamu katika barabara ya Mahiwa na Zigua.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Maadili Kasimu Kumbawene wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Desemba 21, 2024, amesema tatizo lilianzia Oktoba 19, 2024 kampuni ya Bhakharesa iliomba kibali cha ukarabati wa barabara ya Mahiwa na Zigua.
Kwahiyo tunamuomba sana Mama Samia aweze kusitisha zoezi la Jumatatu kwani litakuja kuleta picha mbaya kwa sisi tunanung’unika kwanini tuondolewe sisi tuu utaratibu na busara vitumike na sisi tutafuata utaratibu utakaopangwa.”
Alikuja Mhe. Awadhi kutuomba tuziondoe meza ili ukarabati ufanyike kwa sababu baada ya ukarabati mtapata manufaa na sisi tukaliona hili mingoni mwa wanufaika wa barabara tutakuwa sisi na sisi hatukuona kipingamizi katika hilo tukashauriana na yeye tukaomba sehemu ya kuhifadhi meza zetu akatuelekeza kuhifadhi mbele ya msikiti ambapo kunachuo, baada ya siku tatu kuanzia Juma tatu Desemba 23 na 24 Juma na kufikia jumatano kukaletewa afisa polisi wa jamii na kutuambia hatutaruhusiwa kurudi katika maeneo haya na kule mbele mtaa wa Livingstone na Mahiwa kuliwekwa geti na Mchikichi Zigua kuliwekwa kuonesha kwamba sisi hatutakiwi kurudi na kukaletwa walinzi kampuni binafsi kuzuia sisi tusifanye biashara.
Wafanya biashara hao wakiwa kwenye eneo ambalo wanafanya buashara zao tangu mwaka 1994.Amesema jambo la kwanza kwa sababu wanamahusiano mazuri na Msikiti, tukawafuata viongozi wa Msikiti kuwauliza kuhusiana na hilo jambo,…. Viongozi wa Msikiti wakasema wao hawahusiku hili jambo lipo chini ya Salim Said Bakhresa na huku tetesi zinasema amenunua barabara kwamba hatutakiwa kurudi…
Tukaenda kwa Awadhi tena… Tukaoingea nae zaidi ya vikao vitatu “ Akasema Bakhresa hataki kuona Uchafu.”… Sisi familia zinatutegemea.” amesema Kumbawene
Kwa Upande wa Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mhiwa na Zigua, Ramadhani Ally amesema alipewa taarifa na serikali ya mtaa ili aweze kutoa taarifa ya operesheni ya Jumatatu saa nne kuondoa vitendea kazi pamoja na biashara katika eneo la barabara wanayofanyia biashara.
Pia amesema alifanya jitihada za kumtafuta Diwani pamoja na Mkurugenzi wa Manisppaa kwaajili ya kuomba suluhu juu ya jambo hilo lakini juhudi hiizi hazikuzaa matunda…” Lakini Operesheni ya kutuondo itaendelea kesho
Kwa Upande wa Mwanachama Musa Bin Rehan amesema kuwa kunafitina imeingia katika zoezi hilo, pia kunachoyo imeingia juu ya chuki dhidi ya mwanadamu mwenziwe…. “Chokochoko na Kadhia zote zipo chini ya Awadhi ambaye ni msimamizi wa Msikiti baada ya kuamiwa na Bakharesa kusimaia mahitiji yeyote ya kigharama ya msikiti wa Mtoro lakini kinachoonekana mamlaka aliyopewa yamemlevya amefikia hatua ya kujiona mungu mtu" amesema.
0 Comments