MR.UK KUNGA KIWANDA CHA MAJOKOFU PWANI



Meneja Mtendaji wa Kampuni ya Mr.UK Deo Joachim Kusare  akionesha jiko la gesi moja ya bidhaa babdani hapo huku anayeahuhudia ni  Meneja Masoko wa Hotel Rolex Constancia Makoye. 

Kibaha,Pwani 
Mkoa wa Pwani unatarajia kuwa na kiwanda cha kutengeneza majokofu hii ikiwa ni katika kukuza uchumi wa viwanda.

Akizungumza  na waandishi wa habari  kwenye banda ya Mr.UK Tanzania ambaye ni kati ya washiriki wa Wiki ya Maonesho  ya Viwanda  biashara na uwekezaji  yanayoendelea kwenye viwanja vya Stendi ya zamani Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani  
 
Meneja Mtendaji wa Kampuni 
 Deo Joakim Kusare amesema kuwa wanatarajia  kukamilisha ujenzi wa kiwanda  cha kutengeneza  majokofu ambacho kitakua Kerege Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani  ndani ya miaka miwili ijayo na  tayari ujenzi wa wa kiwanda hicho umeanza

Hivi sasa  Mr.UK ni  Kampuni kubwa  na maarufu kutokana  na biashara yake ya kuuza bidhaa mbalimbali  za vifaa vya ndani vinavyotumia  umeme.

"Biashara  zetu zimejikita kwenye kukidhi haja kwa watu wa kada zote za kipato na hadi sasa runefanikiwa kutoa ajira nyingi kwa vija a nchini"amesema Meneja  Kusare.

Amesema kuwa hivi sasa wanachukua malighafi  kutokanje ya nchi na wanamiliki katakana ndogo iliyopo  maeneo ya Tandale Jijini  Dar es Salaam.

"Hivi sasa  tunachukua malighafi nje ya nchi kisha tunakuja kuunganisha kwenye katakana yetu  iliyopo Tandale  amezitaja baadhi ya bidhaa wanazounganisha kuwa ni  sabufa,sound bar AC,Majokofu pampu za kilimo pamoja na majiko ya gesi yanayotumia kiwango kidogo cha gesi.

Kusare  amesisitiza  kwa kusema kuwa  vifaa vyao  vinapatikana kwa bei nafuu pia vinatumia umeme mdogo .

Wakati huohuo Meneja  Masoko wa Hotel Rolex Constancia Makoye   amesema mbali ya bidhaa hizo   kesho tarehe  20 Desemba, 2024 watazindua hoteli yenye hadhi ya nyota tano itakayo fahamika kwa jina la Rolex ambayo iko Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments