Waandishi wa Habari wameaswa kuandika habari ambazo zitasisitiza umuhimu kwa wananchi kote nchini wanaoendelea na ujenzi wa nyumba zao kuzingatia kutumia wataalamu wenye leseni kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).
Akizungumza jana kwenye mafunzo ya siku moja yaliyoongizwa na Afisa Uhusiano na Mawasiliano Ewura Titus Kaguo pichani juu amesisitiza kuwa kabla ya kuunganisha umeme wa majumbani muhusika anapaswa kutumia mtaalam wa kuweka mifumo ya umeme kwenye nyumba ambaye amesajiliwa na Ewura pindi linapotokea tatizo kama ajali ya moto muhusika alipwe haki zake.
Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JNICC, Dar es Salaam.
Aidha Kaguo amesema kuwa pindi mtu akikumbwa na janga swali la kwanza atakaloulizwa muhusika je wakati anaunganisha umeme wake fundi aliyemuwekea mfumo ana leseni ya Ewura ?
"Janga litakapotokea tutakuuliza je mfumo wako uliwekwa na fundi mwenye leseni ya Ewura jibu la mteja ndilo litatupa njia ya kupata utatuzi wa hiyo changamoto hivyo nawasihi wananchi wote kuzingatia mafundi wenye usajili na siyo kutumia vishoka" amesema Kaguo.
" Ikiwa nyumba yako imeungua halafu umetumia watalaam wa mifumo ya umeme waliosajiliwa na Ewura, unalipwa haki zako bila tatizo tofauti na yule aliyetumia mafundi wa mitaani," amesema Kaguo
Mafunzo hayo ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Kwa wafanyakazi wa Vyombo mbalimbali vya habari Tanzania (JOWUTA) yalimefa Desemba 13, Jijini es Salaam na kuhudhuriwa na Waandishi wahabari 100 kutoka magazetini, luninga, redio na mitandao mbalimbali ya kijamii.
Katibu wa JOWUTA, Suleiman Msuya akisikiliza mada kwenye mafunzo hayo. kwenyemkutano.Msuya ametoa shukrani za dhati kwa Ewura kwa kukubali kutoa mafunzo hayo kwa wanachama wa JOWUTA.
Baadhi ya Wanachama wa JOWUTA wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Wakati huohuo Kaguo amesisitiza wananchi kutambua haki zao hasa Mamlaka ya Maji Dawasco ikiwa ni pamoja na kutokukatiwa maji mwisho wa juma na kupewamalipo stahiki kutokana na matumizi ya mteja na kwamba siyo sahihi msoma mita kukisia ankara ya mte ja.
Baadhi ya Wanachama wa JOWUTA wakiwa kwenye mafunzo hayo.
0 Comments