MAONESHO YA NNE YA VIWANDA KUZINDULIWA DES 17 ,2024 KIBAHA

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema Wiki ya  Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani ambayo inafanyika kwa mara ya nne  yamepangwa kuanza  Desemba 16 hadi 20 mwaka huu huku yakizinduliwa rasmi Desemba 17 mwaka huu yamepangwa kufanyika viwanja vya Mailimoja Kibaha (Stendi ya Zamani)

Akizungumza  na Waandishi wa Habari leo  Desemba 2,2024  kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ofisi za Mkuu wa Mkoa Wilayani Kibaha,  amesema maandalizi  yamekamilika.
"Tumeandaa Wiki ya Viwanda  Mkoa wa Pwani ambapo  maonesho haya yatahusisha wenye viwanda  wa ndanina nje ya Mkoa wa Pwani wanakaribishwa  ili waweze kuonesha bidhaa zao wanazozizalisha"amesema Kunenge. 

Mkuu wa Mkoa ameongeza kwa kusema kuwa maonesho hayo yatafunguliwa na mgeni rasmi ambaye atafahamika baadaye.
Desemba 18, 2024  kutafanyika Kongamano  maalumu lililopangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kwamfipa Kibaha  huku washiriki zaidi ya  550 wanatarajiwa kushiriki  na kujifunza  na kuona fursa mbalimbali  zinazopatikana  Mkoani hapa.

"Kwenye  Kongamano hilo  Viongozi  mbalimbali  kutoka serikalini, Mashirika ya Umma na sekta binafsi na wataalamu wabobevu ,wataalamu wa biashara na uchumi watakuwepo" amesema  Kunenge.
Kunenge  amesema kuwa Mkoa umejipanga vizuri kwa maonesho hayo ya Viwanda na  biashara na wanatarajia
Viwanda 1,553 kushiriki huku  Viwanda 78  vikubwa vimeanzishwa tangu Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  alipoingia madarakani inakadiriwa  watu 25,000  wanatarajiwa kuhudhuria  maonesho hayo

Kunenge  amesema kuwa Mkoa umejipanga vizuri kwa maonesho hayo ya Viwanda na  biashara na wanatarajia
Viwanda 1,553 kushiriki huku  Viwanda 78  vikubwa vimeanzishwa tangu Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  alipoingia madarakani inakadiriwa  watu 25,000  wanatarajiwa kuhudhuria  maonesho hayo

Post a Comment

0 Comments