RAIS MSATAAFU ALI HASSAN MWINYI ATEMBELEA MIRADI MITATU YA NSSF AWAMWAGIA SIFA

 Mkurugenzi wa  Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF, Ramadhan Dau  (kushoto ) akimueleza jambo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili , Alli Hassan Mwinyi  aliyesimama katikati ni Waziri wa Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka .(PICHA  ZOTE NA MICHUZI MEDIA GROUP)
 Sehemu ya ujenzi wa  nyumba ukiendelea Dege Kigamboni.

Kutoka kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alli Hassan Mwinyi akiingia  katika moja ya ofisi  katika daraja la Kigamboni akifuatiwa na Mkurugenzi wa NSSF, Ramadhan Dau na Waziri wa Kazi  na Ajina Gaudensia Kabaka.
 Injinia Karim Mataka akitoa amelezo kwa rais Msataafu .
 Mkurugenzi wa Shirika la NSSF , Ramadhan Dau akimkaribisha  Rais Mstaafu na  katika ofisi zilizopo kwenye mradi wa daraja la Kigamboni ambako alipata amelezo juu ya ujenzi wa daraja hilo litakaokamilika Julai mwakani.
Hivi ndivyo kitakavyokuwa muonekano halisi wa ECO  Village.


RAIS Mstaafu wa awamu ya pili Alli Hassan Mwinyi ameumwangia sifa uongozi  wa Shirika la Hifadhi ya Jamii nchini NSSF, kwa kuwa wabunifu  katika kubuni miradi  yenye ubora ambayo inaendeleshwa  katika maeneo ya Kijichi na Kijiji  cha Dege (Dege Eco Village), kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Mwinyi aliyasema hayo  jana Jumamosi alipotembelea  miradi hiyo kwa mara ya kwanza  ambapo alionekana kuvutiwa sana  na kusema “Nimeshukuru  kupata  nafasi hii ya kutembea miradi mitatu ya NSSF kuanzia ujenzi wa daraja la Kigamboni , ujenzi wa nyumba za Kijichi na kijiji cha Dege  wallah nimesikia raha” alisema Mwinyi. 
Aliongeza kwa kusema kuwa anawapongeza  NSSF kwa kuwa na fikra yakinifu ambazo zimezaa matunda ya kujivunia katika serikali , ni jambo la fahari  kwa nchi yetu  kwani haya ndiyo amendeleo ambayo tuliyokuwa  tunayaota siku zote.

Mwinyi aliongeza kwa kusema kuwa ifike wakati  watanzania waachane na  maisha ya kuishi  kinyonge na katika nyumba ambazo ni za kimasikini na zisizokuwa na hadhi  ya kuishi binaadamu.

Nina imani kubwa kwamba ipo siku watu wanaoishi Manzese, Buguruni na kwingineko watahama  na kuhamia katika nyumba za bei nafuu za mradi huu wa Dege na Kijichi na haya ndiyo maendeleo yenyewe.

Aidha alisema kwamba tofauti iliyopo katika nyumba hizo ni  bei na gharama hivyo mtu ataweza kuishi kwa nyumba ambayo ni kubwa ama ndogo ya kiasi cha familia anayohitaji .


“Narudua tena kuwa nawapongeza  viongozi wa NSSF wakiwa chini ya Mkurugenzi wao Ramadhan Dau  kwa kuwafikiria yaliyomema Watanzania waliowengi kwa kujenga nyumba zaidi ya 7,000 pia nawaombea maisha marefu na yenye afya njema”, ifike wakati Watanzania wote waishi katika hali ya maisha ya kufanana hasa katika makazi na tofauti itakuwepo katika kipato cha kila mmoja tu  na siyo mahali pa kuishi” alisema Mwinyi.

Akiuzungumzia mradi wa daraja la Kigamboni alisema kwamba jana ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza  kwenda kutembelea mradi huo na kuahidi kuwa katika mstari wa mbele  katika kuchangia hasa kwenye ulipaji  katika kuvuka pindi kivuko hicho kitakapokamilika Julai mwakani.

Alimalizia kwa kusema kuwa anakumbuka wakati alipokuwa  madarakani aliweza kutembelea nchi ya Netherlands ambako walikuwa waking’oa madaraja yao nay eye akapafikiria sana Kigamboni lakini alipowaomba madaraja ili wampe pamoja na wajenzi wao wakamwambia kuwa alichelewa kwa sababu walikwisha  yagawa madaraja hayo kwa  makoloni yao hivyo  anaona  ujenzi wa daraja hilo umetimiza njozi yake.
Baadhi ya wanahabari katika ziara hiyo. 

Post a Comment

0 Comments