KIBAHA SHOPPING MALL KUZINDULIWA KESHO DES 7,2024

 Mhasibu  wa Halmashauri ya Mji Kibaha  Luna  Kakuru.

Kibaha, Pwani

Mhasibu wa Halmashauri ya Mji Kibaha  Luna Kakuru amesema  kuwa ndani ya soko hilo la kisasa (Mall) wafanyabiashara mbalimbali  wamepata fursa  za kupangishwa na  vyumba vyote vimejaa.

Tutakuwa na wafanyabiashara wenye nembo  zote kubwa hapo baadaye pamoja na huduma  za kibenki nazo zitapatikana hapa hivyo wakaazi wa Kibaha na viunga vya jirani watapunguza gharama za kuingia mjini.

 Kakuru amesema  huduma zingine zitakazopatika ni pamoja na  michezo ya watoto, kutakuwa na huduma  watoa vyakula na vinywaji mbalimbali (bar).

"Huu ni mradi wa  kimkakati  pia matarajio yetu ni kukusanya kiasi cha Mil.660 kwa mwaka" anesema Kakuru.
"Tunamshkuru  Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha mojakwamoja kufanikisha mradi huu ambao umekamilika mwaka jana" amesema Kakuru.

Mfanyabiashara Charles   Chandika ambaye  ni mmiliki waduka  la   bidhaa za kilimo na mifugo amewahakikishia  wakaazi wa kibaha  kupata huduma  bora.

Wasanii mbalimbali  watapamba uzinduzi  huu ambao ni kundi la Weusi, Maarifa,Smata.
Afisa Biashara wa Halmashauri ya Mji Kibaha Sabrina Kikoti amesema kuwa 
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon   atakua mgeni rasmi kwenye uzinduzi  wa soko la kisasa litakalofahamika kwa jina la 'Kibaha Shopping Mall' utakaofanyika kesho tarehe 7Desemba , 2024.

Akizungumza  na Waandishi  wa Habari   mchana wa leo  tarehe 6,Desemba ,2024  Afisa Biashara  Halmashauri  ya Kibaha  Kikoti amesema kuwa  kwa niaba ya Mkurugenzi  wao  wanatoa shukran kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa uwekezaji  mkubwa alioufanya  wa soko hili.

"Ujenzi  wa soko hili umegharimu kiasi cha  Bil.8 fedha ambazo zimetoka serikali kuu" amesema Sabrina.
Taswira ya Kibaha Shopping Mall  inavyoonekana kwa mbele.

Post a Comment

0 Comments