Na Mwandishi Wetu, Kibaha
MWENYEKITI wa Mtaa wa Muharakani uliopo eneo la Mkuza Wilayani Kibaha Mkoani Pwani amezungumza adha wanayokabialiana wanachi wake ya changamoto ya barabara kwa miaka kumi sasa.
Mwenyekiti huyo Mohammed Ally Mohammed amesema awali akichukua jitihada za kwenda kuulizia kwa nini ujenzi wa daraja hilo dogo karavati umesitishwa na kuachwa bila kukamilika akajibiwa kuwa Mkandarasi hajalipwa.
Akizungumza juu ya adha wanayoipata wananchi wa eneo la Muharakani Mtaa wa Filbert Bayi Picha ya Ndege Kibaha Moses Sawe amesema kuwa wananchi wanahitaji barabara yao ichongwe ili magari na wananchi waweze kupita kwa urahisi tofauti na ilivyo sasa.
"Tunashangazwa sana kuona kuna baadhi ya mitaa wanapatiwa huduma za ujenzi wa barabara tofauti na ilivyo huku kwetu" amesema Sawe.
"Katika ujenzi wa karavati haujakamilika ipasavyo kwani ameondoka bila kujaza kifusi hali inayopelekea karavati kuwa dhaifu huku kwenye kingo kukitengeneza makorongo na kuhatarisha zaidi waenda kwa miguu na vyombo vya moto" amesema Sawe.
TARURA Wilaya watueleze ni lini hii barabara itatengemaa tunawaomba watoke maofisini waje kuona hali halisi.
Mzee Laurian Phabian Mtundabyema anayeishi hapo tangu mwaka 1998 amesema kuwa tunahitaji barabara yetu ichongwe kwani ni zaidi ya miaka kumi tangu ichongwe.
"Mbunge wa Kibaha Mjini Sylivestry Koka hajaja huku tangu alipoingia madarakani asisubiri kuja katika kipindi cha uchaguzi kuomba kura zetu hatutamwelewa" amesema.
MamaJoseline Emmanuel amesema kuwa eneo hilo limekuwa kero kubwa kwa wakina mama , watoto na vijana huku amesisitiza kwa kusema kuwa watoto wanashindwa kwenda shuleni na njia kuwa ndefu kutokana na uharibifu wa njia hiyo ambao umezidishwa na mvua zilizopita.
"Kipindi cha mvua tumeteseka sana na inatugharimu kuingia gharama kubwa za usafiri wakati mwingine hata waendesha pikipiki hugoma" amesema.
Bibi Paulina Mayunga (81) amesema kuwa kwa niaba ya wazee wenzake wanateseka huku amemuomba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan awasaidie.
Aidha Mohammed Lukemo(83) ambaye ambaye ni mkaazi wa eneo hilo tangu 1964 amsema matatizo katika barabara hiyo yameanza muda mrefu.
Wakati huohuo mkaazi wa eneo hilo la Muharakani Felix Swai amesema kuwa hivi karibuni alikwenda kutoa malalamiko yake TARURA Mkoa wa Pwani ,"hili eneo barabara ni ya muhimu sana na wanapaswa kuitengeneza barabara hii ambako kuna uwekezaji mkubwa wa shule ya Filbert Bayi kuanzia chekechea Shule ya Msingi hadi Sekondari kadhalika kuna Hospitali yenye hadhi ambayo inamilikiwa na Meja Mstaafu wa JWTZ pia aliyekua mwanariadha nguli aliyeandika rekodi katika miaka ya 1980's na aliyeacha alama katika ulimwengu wa michezo ya kukimbia duniani Filbert Bayi.
"Timu za mbalimbali za michezo hupiga kambi, michuano ya michezo na makongamano mbalimbali hufanyika lakini njia ni mbovu na wakati wote Bayi amejitolea kutengeneza lakini peke yake hawezi serikali ishughulikie"
Meneja TARURA Wilaya ya Kibaha Samuel Ndovani amesema kuwa wanatambua chagamoto ya eneo hilo huku akisisitiza kwamba tayari ameshatuma wataalamu wamefika katika eneo hilo na kulifanyia tathmini kwa kina.
"Wataalamu wa TARURA Wilaya ya Kibaha wamefika eneo lenye changamoto kuhusiana na barabara ya Jamaika kuelekea Filbert Bayi hivyo naahidi barabara hiyo itachongwa sababu Mkandarasi tunaye kazi itaanza wiki ijayo" amsema Ndovani.
Mama Joseline Emmanuel amesema kuwa kutokana na changamoto hiyo wanawake, vijanana watoto wanataabika kwenda shule na katika shughuli mbalimbali za utafutaji riziki.Bibi Paulina Mayunga mwenye umri wa miaka (81) amesema yeye pamoja na wazee wenzake wanapata taabu sana kwa kutopitika kwa barabara hiyo.
Mkaazi wa eneo hilo la akionesha namna karavati hilo lilivyo haribika.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mharakani Kibaha pichani juu Mohammed Ally Mohammed amesema amejitahidi kufuatilia utauzi wa chagamoto hiyo na kusema anaomba Viongozi wawatatulie wananchi kero hiyo.
Felix Swai aliyekaa katikati akifafanua jambo kuhusu barabara hiyo ya Filbert Bayi
Mzee Mohammed Lukemo (83) amesema yeye ameanza kuishi katika eneo hilo tangu mwaka 1964 na limekua na historiaya kutopatiwaufumbuzi.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Kibaha Samuel Ndovani ambaye amewahakikishia Waandishi wa Habari kuwa watakwenda kutatua changamoto hiyo ya wakaazi wa eneo la Jamaica kuelekea Shule ya Filbert Bayi,Mkuza Kibaha ndani ya wiki moja.
0 Comments