UMOJA WA ULAYA KUSHINDANISHA VIJANA WA TANZANIA

Kutoka kulia ni Mratibu wa Tamasha la Umoja wa Ulaya Mosse Sakar katikati Ofisa Uhusiano wa Umoja wa Ulaya Sara mbise na Ofisa Mawasiliano na Uhusiano  Bodi ya Filamu nchini Tanzania wakizungumza na waandishi wa habari jana kwenye uzinduzi wa tamasha hilo ambalo  mwaka huu limekuja kivingine kwa kutoa fursa kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 kutunga filamu fupi itakayochezwa kati ya dakika 5 hadi kumi itakayohusu  kuongez3ka kwa idadi ya watu duniani faida na hasara zake kwa kuwa ongezeko hilo inagusa  sehemu nyingi katika maisha ya kila siku pia nia agenda ambayo VIJANA nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya  mashindano yatakayofanyika kwa mara ya kwanza ya uandishi  na uchezaji wa filamu fupi itakayoelezea faida  au hasara ya ukuaji wa idadi ya  watu duniani.

Shindano hilo limepangwa kuwashirikisha vijana  wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 ambao wana njozi za kufanikiwa kwenye tasnia ya filamu  na ambao hawajawahi kufahamika kabisa.

Akizungumza jana na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa shindano hilo uliofanyika kwenye Ofisi za Umoja wa nchi  Ulaya Ofisa habari wake   Susan Mbise alisema  shindano hilo ni la hiari na watakaopenda kushiriki watatakiwa kujaza fomu maalumu.

"Shindano hili limeandaliwa  ili kuwapa wasaa vijana kuweza kuonesha vipaji walivyo navyo ambapo kila mmoja atatakiwa kurekodi filamu kwa lugha ya kiswahili pamoja na 'subtittle'za kiingereza" alisema Mbise.

Aidha aliweka wazi kuwa shindano hili linawahusisha vijana wa nchi nzima na  filamu hiyo itatakiwa kuwa ndani ya muda wa dakika tano au kumi .

 Baada ya hapo filamu 15 bora zitaoneshwa  kwa umma ambao baadaye  zitachaguliwa filamu tano bora huku mshindi wa kwanza akijinyakulia kitita cha  Sh. Mil.7 , mshindi wa pili atapata Sh. Mil.5 na watatu ataondoka na Sh. Mil.3.

Pia kutakuwa na zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kujifunza lugha ya Kifaransa kwenye kituo cha utamaduni cha Ufaransa Jijini Dar es Salaam.

Naye Mratibu wa shindano hilo Kutoka Kampuni ya Anderson Macha Mosse Sakar alisema  zaidi ya miaka 25 Umoja wa Ulaya wamekua wakifanya tamasha hilo halikua lenye mafanikio huku akisisitiza vijana wajitokeze kwa  wingi.

Wakati huohuo Ofisa Mawasiliano  Uhusiano Bodi ya Filamu Abuu Kimario  alisema tamasha hilo limekuja katika wakati muafaka na kupongeza Umoja huo  kuelekeza nguvu kwa vijana wachanga.

"Hivi sasa lugha ya Kiswahili imekua lulu duniani  hivyo vijana  watakaopata  nafasi  ya kushiriki  wataweza kuitangaza vyema  nchi yetu ya Tanzania" alisema Kimario.

Alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa anawaasa vijana  kutumia muda huu kujifunza viwango vya Kimataifa  pamoja na kuzingatia masharti na vigezo.

Fomu zinapatikana kwenye kituo cha utamaduni cha Ufaransa, Brithish Council  washiriki wametakiwa kurudisha fomu  hizo mara  baada ya kuzijaza kabla ya Juni 15 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments