Akina mama waombolezaji wakisawazisha
kaburi la marehemu Sinjembele Julius(62) aliyeuawa kwa kupigwa na mwanae Ndele
Julius(25).
Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia mazishi ya Sinjembele yaliyofanyika Nyumbani kwake katika kitongoji cha Igawilo kata ya Swaya Mbeya.
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya firauni, unaweza kusema hadithi kumbe nikweli ,Mkazi
wa Swaya jijini Mbeya Ndugu Ndele Julius amemuua mama yake mzazi kwa kumpiga
mateke na ngumi kisha kutoroka pasipo julikana Novemba 25 mwaka huu.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 10
jioni nyumbani kwa mama huyo mara baada ya kutokea kwa ugomvi kati ya mtoto
wake na kijana mwingine hali
iliyopelekea mama huyo kuingilia ndipo alipo kutwa na mauti huo.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa
Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani
amesema kuwa Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliokuwepo kati ya mtoto wake na
kijana mwenzake kitendo ambacho
kilipelekea mama huyo kuingilia ugomvi huo .
Amesema wakati mama huyo akijaribu kuamulia ugomvu huo mtoto
wake alicha kupigana na mwenzake na kuanza kumshambulia mama yake kwa kumpiga
ngumi na mateke mwilini.
Amesema mama huyo alifariki muda mchache
kutokana na kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababishiwa majeraha
makuibwa yaliyopeleka kupoteza uhai wake.
Awali akizungumzia tukio hilo Mtoto wa
Kwanza wa mama huyo Ndugu Razaro Mbwiga amesema kuwa mdogo wake alikuwa na
tabia ya kugombana na mama yake marakwamara .
Hata hivyo teyari mwili huo umekwisha
chukuliwa hospitali na kuzikwa ambapo katika maziko hayo Chama cha Muungano wa
kijamii (Mujata) umewataka vijana kujiepusha na vitendo viovu kama uvutaji
bangi na pombe za kienyeji kwani ndio chanzo cha kutokea kwa vurugu nyingi. Mjengwa.
0 Comments