Mkurugenzi Mtendaji wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire akiwa na Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Pwani Beatrice Kasimbazi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akisalimiana na Naibu Waziri wa Maji Kundo Mathew leo Januari 7,20205 mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Mkoani hapa.Mhe.Kundo Mathew (Mb) akisaini kitabu cha wageni kwenye Ofisiya Mkoa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Pwani Zainab Vullu.
Kibaha,Pwani
Naibu Waziri Wizara ya Maji Mhe. Kundo Mathew amesema kuwa serikali imetenga Kiasi cha Bil.8 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji katika eneo la Pangani Wilayani Kibaha na tayari Mkandarasi ameshapatikana hivyo wananchi wa Kata hiyo wataenda kuondolewa adha ya muda mrefu ya ukosefu wa maji .
"Napenda kutoa ahadi kwamba ifikapo Aprili mwaka huu mradi huu utakwenda kutekelezeka ikizingatiwa kuwa maji ni uhai na hitaji mujimu kwa kina mama nafamilia nzima kwa ujumla" amesema Mhe. Kundo
Naibu Waziri Kundo amesema hayo leo alipokutana na Mamemeja wa Mamlaka ya Maji safi Dawasa huku amewasisitiza kujenga uhusiano mzuri na wananchi ambao ndiyo wateja wao wakuu.
Mhe.Kundo amesema hayo leo kwenye kikao kazi cha kukumbushana yake wanayoyapata kwa wananchi ikiwamo namna ya kutoa huduma bora kwa wananchi .
Kikao kazi hicho kimewakutanisha viongozi wa wakuu wa Idara mbalimbali za Dawasa, Ruwasa iliyofanyika leo Kibaha Januari 7 kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Kundo amesema kuwa wananchi Dawasa wanao wajibu wa kutoa elimu ya ni nini kifanyike katika kutatua changamoto zinazojitokeza huku akisisitiza wananchi kupewa taarifa kabla ya kukatiwa huduma ya maji.
"Tuendelee kujenga mifumo ya maji taka kwa sababu sisi kama serikali hatutaki kuzunguka na magari hivyo tukajenge mifumo ya maji taka.ambayo itakwenda moja kwa moja sehemu husika inayopokea maji taka
wanachohitaji ni kuona serikali yao inawajali kiasi gani kwa sababu serikali iko mlangoni kwao.
'Jengeni mtandao wa maji kufuatia maelekezo ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Dawasa Mhandisi Mkama Bwire amesema kuwa wanajivunia kwa kuwa ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wameweza kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji ambao umeongezeka kutoka lita 153,649, 000 hadi lita 183,649,000
sawa na ongezeko la lita 30,000,0
mtandao wa usafirishaji na usambazaji maji umeongezeka kutoka Kilomita 4,690.7 hadi Kilomita 7,087 sawa na ongezeko la Kilomita
1,396.3 huku mtandao wa maji taka umeongezeka kutoka Kilomita 450 hadi Kilomita 519.4 sawa na ongezeko la Kilomita 69.4.
Mhandisi Bwire amesema kuwa idadi ya wateja wa maji safi imeongezeka kutoka 343,019 hadi 438,177 sawa na ongezeko la wateja 95,158 na kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma ya maji safi katika wastani wa asilimia 89 hadi asilimia 93 na huduma ya usafi wa mazingira kutoka asilimia25 hadi 45.
"Mafanikio mengine ni pamoja na kuanza utekelezaji wa bwawa la Kidunda lenye mkataba wenye thamani ya Bil.335.9 hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 25.7, kutolewa kwa kibali cha kuanza maandalizi ya mradi mkubwa wa kutoa maji kutoka mto Rufiji ambapo utatosheleza mahitaji ya maji ifikapo mwaka 2052 utekelezaji wa kuandaa michoro ya mwisho pamoja na kuandaa nyaraka za manunuzi umefikia asilimia 88" amesema Bwire.
Mkurugenzi Bwire ameongeza kwa kusema kuwa uwezo wa uzalishaji maji umeongezeka kutoka lita 520,000,000 kwa siku hadi lita 534,600,000 kwa siku na ongezeko la lita 14,500,000 kwasiku.
"Dawasa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwani pamoja na mabadiliko ya tabia nchi na kuainisha kuwa elimu kwa wananchi inahitajika juu ya utunzaji wa mazingira,uvamvamizi na uharibifu wa vyanzo vya maji na kuwasisitiza umuhimu wa upandaji miti huku akisema kuwa tayari miti 15, 000 imepandwa" amesema Mhe. Bwire.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa elimu kwa umma inahitajika kuhusu umuhimu wa wa kulipa ankara za huduma ya maji.
0 Comments