UMISSETA MKOA WA DAR ES SALAAM WAPAMBA MOTO

Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam N Edward Otieno akizungumza wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Lipesi Kayombo akiwasalimu wanamichezo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam  katika Uwanja wa Uhuru.
Baadhi ya wanamichezo kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam wakifatilia mchezo kati ya Ilala na Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam  katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na mchezaji wa Mpira wa Miguu Manispaa  ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Lipesi Kayombo (Kushoto), Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam Edward Otieno (Katikati) na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Khamisi Lissu wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam katika Uwanja Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Lipesi Kayombo akitoa hamasa kwa timu ya UMISSETA Wilaya ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam  2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiimba wimbo maalumu wa Michezo ya UMISSETA wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es Salaam 2017 katika Uwanja wa Uhuru.

Na Mathias Canal

Maandalizi ya ngazi ya Mkoa wa Dar es salaam Kwa Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania yamezidi kupamba moto katika Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es  Salaam.

Maandalizi hayo kwa ngazi ya Mkoa kwa ajili ya kupata timu ya Mkoa wa Dar es salaam yameanza kwa kushirikisha timumkutoka Manispaa za Mkoa ikiwemo Ilala, Temeke, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo Kwa ngazi ya Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam Kaimu Katibu Tawala  Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam  Edward Otieno amewasihi washiriki kutumia weledi wao wa mafunzo waliyoyapata kuhusu michezo na kuonyesha umahiri wao ili kuchaguliwa katika timu ya Mkoa.

Wanafunzi hao ambao wameweka kambi katika Shule ya Sekondari Jitegemee mpaka Mei 31, 2017 wataanza safari ya kuelekea Jijini Mwanza kwa ajili ya mashindano hayo ngazi ya Taifa yanayotaraji kuanza kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba June 6, 2017.

Otieno alisema kuwa vijana hao wanapaswa kutambua kuwa michezo ndio ajira inayolipa zaidi duniani hivyo wanapaswa kudumisha nidhamu kwa kipindi chote cha mashindano.

Aliongeza kuwa wanapaswa kutambua kuwa timu zote za Mkoa wa Dar es Salaam zitakwenda Mwanza kushindana katika michezo hiyo ngazi ya Taifa na si kushiriki pekee.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo  John Lipesi Kayombo aliyezuru katika Uwanja wa Uhuru kujionea timu ya vijana wake kutoka Manispaa ya Ubungo ikichuana vikali na timu ya Manispaa ya Ilala amepongeza juhudi za washiriki wote ambao wameonyesha nidhamu ya hali ya juu.

"Ukiona vijana wana nidhamu kama hivi ni vyena kuwapongeza na kuwatia moyo maana bado wana safari ndefu kimichezo "alisema.

Post a Comment

0 Comments