Wasanii wa bendi ya Cocodo wakiwa jukwaani ambao hupiga muziki wao katika miondoko ya asili
Picha Zote na Sauti za Busara.
Cocodo watoto wa Kinondoni waliopania
muziki wa Asili
BENDI ya
muziki wa dansi wa asili ya Cocodo (Cocodo African Music Band) wametoa wito kwa
wanamuziki wa hapa nyumbani kujifunza zaidi muziki kuliko kuingia katika muziki
kwa kusema kwamba tuna kipaji.
Kuwa na
kipaji sawa lakini kipaji bila kusoma kamwe muziki wa hapa nyumbani
hautafanikiwa kusonga mbele na kuwa wa Kimataifa.
Cocodo ambao
walionyesha vipaji vyao katika tamasha la Sauti za Busara siku ya sikukuu ya Wapendanao(Valentine Day)
kwenye tamasha hilo lililofanyika katika viwanja vya Ngome Kongwe Zanzibar.
Hayo
yalisemwa na Kiongozi wa bendi hiyo Remigius Sostenes kwamba hii ni mara ya
kwanza kwa bendi hiyo kupata fursa ya kutumbuiza katika tamasha hilo la 12 la
Sauti za Busara hivyo wakajiandaa kuitumia fursa hiyo kwa kujitangaza kwa sababu
katika tamasha hili kuna wadau mbalimbali kutoka katika mataifa mbalimbali kutoka
nje ya nchi ambao hufika kuangalia vipaji na wengine kupeleka sifa nzuri za wasanii ambao waliweza kuwaona
katika tamasha na kuvutiwa kufanya kazi nao kwa kuwatumia mialiko.
“Hapa tuko
sokoni hivyo na sisi tulipopata taarifa kwamba tutakuwa miongoni mwa washiriki
tukajiandaa kujitangaza kwa kutoa burudani nzuri kwa wahudhuriaji” anasema
Sostenes.
Akizungumzia
jinsi bendi yao ilivyoanza anasema kwamba bendi hiyo ilianzishwa na wasanii
wachache lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele bendi iliongeza idadi ya
wasanii ambao wote waliokuwa wakiomba kujiunga nao walikuwa na vipaji.
“Tulianza
kufanya sanaa ya muziki bila kuusoma hiyo ilikuwa 2010” anasema Sostenes.
Changamoto za bendi
Kwa upande
wa changamoto Kiongozi huyo anaweka wazi kwamba kipato ni kikwazo kikubwa kwao lakini
hawakati tamaa huku wakijaribu kujikwamua na kupambana na changamoto hizo.
“Ilifika
wakati tukawa tunakata tamaa ya kuendelea na bendi lakini dhamira
ikatushinda hivyo tukaamua wote kwa pamoja kutokata tamaa katika sanaa huku
tukiwa na imani kubwa kwamba ipo siku tutafika mbali na kufanikiwa” anasema.
Aisha anaongeza
kwa kusema kuwa wamekuwa wakipata mialiko
ya kushiriki katika matamasha mbalimbali nje ya nchi lakini wamekuwa
wakishindwa kwa sababu wamekuwa wakiambiwa wajigharamie kwenda na wakifika
watarudishiwa gharama zao walizozitumia lakini wamekuwa wakishindwa kufanya
hivyo kwa sababu ya kukabiliwa na ukata.
“Tumekuwa na
kiu kubwa ya kushiriki kwenye matamasha hayo
makubwa lakini tatizo ukata ndiyo unaotukwamisha na kushindwa kushiriki
kwenye matamasha ya Kimataifa duniani hivyo tunaomba mashabiki na wadau
watusaide”anasema Sostenes.
Anaainisha matamasha ambayo waliwahi kushiriki ni pamoja
na tamasha la nchi za Majahazi Ziff waliloshiriki kwa misimu miwili Karibu Festival lililofanyika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani. na
Aidha
anaongeza kwamba hawana wafadhili wa bendi yao hivyo wamekuwa na utaratibu wa
kusapotiana wenyewe kwa wenyewe ambapo mwenzao akikwama kwa njia moja ama
nyingine huwa wanamsapoti kwa hali na mali bila kuchoka na hiyo ndiyo siri
kubwa ya wao kuweza kufika hapo walipo hadi hivi sasa.
Anaendelea
kwa kusema kuwa lengo lao kubwa ni kuweza kufika mbali katika tasnia ya muziki
na kuitangaza nchi kwa ujumla kwa kupitia matamasha makubwa ya kitaifa na
kimataifa.
Nini
kilichowavutia bendi ya Cocodo kuimba
muziki wa asili?
Sostenes
anasema kutokana na umri walio nao wangekua wamebobea katika kuimba muziki wa
kizazi kipya Bongo Fleva lakini wamejikita katika muziki wa asili kwa sababu moja kuu ni
kutafuta lebo ya asili katika muziki wanchi hii.
Kabla ya
kuamua kuimba muziki katika miondoko ya muziki wa asili tulikuwa tukipiga miziki mbalimbali ya kukopi lakini mwisho wa siku ndipo
tukaamua kupiga aina moja ya muziki ili iwe rahisi kutambulika zaidi kama jinsi ilivyo hivi sasa anasema
Sostpeter.
Bendi ya
Cocodo inapiga muziki wake katika
mahadhi ya Kitanzania na Kiafrika pia hupiga muziki wa aina ya Jazz huku mtindo wanaopiga muziki wao wakiuita kwa
jina la ‘Panyenje Style’ maskani yao ni maeneo ya Mahakamani Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Historia fupi ya bendi ya Cocodo
Bendi hii ya
Cocodo ilianzishwa 2010 na katika nyimbo zao wamekuwa wakitoa ujumbe
mbalimbali zinazohusu mafunzo kwa jamii
kutoa tahadhari ya mambo mbalimbali yanayoikabili jamii ikiwa ni pamoja na magonjwa kama vile
Malaria na Ugonjwa wa Upungufu wa Kinga Mwilini (HIV),vilevile huimba kuhusu
ukuaji wa uchumi wanchi.
Ala za
muziki wanazotumia ni pamoja na zile za asili kama Marimba,Djembe,Zeze huku ala
za kisasa ambazo ni gitaa, kinanda.
0 Comments