POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ! KASHINDWA KUWIKA STUTTGART KISA NA MKASA ?!

 Huu ndiyo ukumbi ulioharibiwa ambako shoo ilitarajiwa kufanyika.
Gari ya Polisi nchini Ujerumani  likiokoa Diamod asipigwe.

POLISI nchini Ujerumani wamemuokoa  msanii wa muziki kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond’  kutoka kwa mashabiki  wenye hasira bada ya kuchelewa kuingia ukumbini Stuttgart.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka nchini Ujerumani  kilisema kwamba  mashabiki wake waliingia ukumbini kuanzia saa nne usiuku lakini jambo la kushangaza ni msanii huyo kuingia ukumbini alfajiri ya saa kumi.
Imedaiwa kwamba Diamond amepelekwa nchini humo na Promota wa Kinaigeria ambaye naye aliingia mitini huku DJ akichezea kichapo kwa madai kwamba  vyombo  vilikua vibovu.

 Pia Tanzania Daima ilijiridhisha kwa kuingia katika mtandao  kijerumani na kukuta  na kichwa cha habari kilichoandikwa  katika lugha ya kijerumani  kikisema Blaulicht aus der Region Stuttgart 31. August: "Diamond Platnumz" zieht Ärger der Fans auf sich.

Tukuio hilo ambalo lilitoakea Agosti 30 2014, majira ya saa 10 alfajiri. Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva Diamond Platnumz alijikuta katika  wakati mgumu hadi alipookolewa na Polisi mjini Stuttgart,Ujerumani.
Aidha baada ya mashabiki waliokuwa na hasira na  kuchoka kusubiri shoo  hiyo huku wakiwa wamelipa kiingilio cha tiketi kwa gharama ya Euro 25 kwa kiingilio walitangaziwa kuwa shoo ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na Promota wake raia wa Nigeria anayefahamika kama Britts Event.
Hapo ndipo mashabiki  walipoona  kuwa hawakutendewa haki hivyo walianza  kurusha  chupa  na kutaka  kumvamia  mwanamuziki  Diamond  na Promota wake.Kilichowakera  zaidi  mashabiki  ni pamoja  na sauti mbovu za  vyombo  vya muziki vilivyofungwa  katika ukumbi  huo jambo ambalo liliwafanya  mashabiki kuvunja hadi vyombo hivyo vya muziki.
Kama hiyo hiyo haitoshi pia Ma Djs nao walichezea kichapo  na wako hospitalini  kwa sasa huku mmoja wao akijikuta akipoteza kompyuta mpakato yake huku mwanadada  Flor alipatwa s mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, mashabiki hao  wanadaiwa kumpa  kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospitali.
Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili  ni la aibu  na halijawahi kutokea, kwa msanii kuchelewa kufika jukwaani  na kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani mashabiki wa  nchini humo  wanaheshimu sana muda wao. Mpaka sasa Polisi wanamsaka Promota wa onyesho hilo na wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashtaka Promota huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Ili kujiridhisha na sakata hili Bongoweekend ilimtafuta Promota wa Diamond hapa nchini Tanzania  Babu Tale ambaye alikiri kwa kuwa sakata hilo ni kweli limetokeakwa kusema .
"Ni kweli fujo zilitokea ambako Diamond hana makosa , yeye alipelekwa na Promota mmoja raia wa Nigeria  hivyo yeye alikua kila akiuliza muda alikua akiambiwa bado na Promota huyo" alisema Tale.
Aidha Tale alikwenda mbali kwa kuongeza kwamba Mapromota wengi wanapoandaa shoo huwa wanaangalia mwitikio wa mashabiki licha ya kwamba shoo hiyo ilipangwa kuanza mapema saa nne za usiku, lakini kwa taarifa nilizozipata  mashabiki walianza kujaa ukumbini saa saba usiku hivyo Promota akaamua kumfuata alipokua Diamond ni umbali wa saa moja hali ambayo ilichangia kupoteza saanzima njiani hadi anafika ni saa tisa usiku nakuanza kuweka sawa mambo ikawa saa kumi alfajiri ndipo kukazuka tafrani hilo ila Diamond yuko salama, alimalizia kwa kusema . 

Post a Comment

0 Comments