‘Ngariba ukimpa mtoto atamfanya vyoyote atakavyo’
Na Bryceson Mathias
KUTOKANA
na watanzania nchini kupoteza Imani na Jeshi la Polisi kila Kona ya
nchi, kuwa linakisaidia Chama Tawala (CCM), huenda Kauli ya Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, ya kulipa Jeuri Jeshi hilo kuwa, liwapige tu wasiotii
amri waumechoshwa; litamsababishia kulia Tena!.
Na Bryceson Mathias
Kauli
ya Pinda imesemewa mahali palepale aliposemea awali kuhusu wanaoua
walemavu wa Ngozi (Albino) kuwa nao wauawe, na alipogeuziwa kibao na
watoa hoja wa eneo hilo hilo aliloko, alilia kwa uchungu na kujutia
Kauli ya Ulimi wake, jambo linaloonesha litamrejea!
Kwa
kuwa Pinda ni Msimamizi Mkuu wa Shughuli za Serikali bungeni, wananchi
hawaoni kama Pinda kasema, ila wanatafsiri kwamba hiyo ndiyo Kauli ya
Serikali ya sasa na Muundo wake (Mfumo), na kuwa sasa itakuwa mtu
asipotii Sheria bila Shuruti ni kupiga tu! Tumechoka!.
Lakini
kibaya kinachojitokeza, Pinda katamko kauli hiyo nzito kwenye chombo
kikuu cha kutunga sheria kati ya Mihimili mitatu (Utawala, Mahakama na
Bunge), hivyo watu wanahisi Taswira hii; ‘Kama anaweza kutoa Kauli hiyo
nzito hadharani, akiwa kwenye vikao vya siri Je!
Wadau
wengi wanapohojiwa Sirini ni wapi wanadai, Kwenye Vikao vya Mikakati ya
Uongozi ndani ya Itikadi yake, Halmashauri Kuu, Kamati Kuu, huku
wengine wakisema, Pinda hajui Ugeugeu wa Polisi, linaweza kuanza
utekelezaji kwa nguvu wakisingizia kasema Waziri Mkuu.
Jambo
kubwa linalowauma watanzania wengi waliosikia Kauli ya Pinda na
Michanngo mbalimbali, hasa baadhi ya Wasomi na Watalaam wa Uchumi
wanasema,”Pinda katoa Kauli hiyo wazi mno, na kwamba, Vyombo vya Habari
na vya Haki vya Kimetaifa vimemsikia.
“Awali
Waziri, Bernard Membe, alilalai ati kuna watu wanadiriki kushawishi
Wawekezaji Nje, ili inyimwe misaada kwa kukosa uzalendo na nchi yao”.
Wanahoji, kwa tamko la Pinda, Wawekezaji wakisitisha Misaada Tanzania,
Mchawi ni Nani?
Pia
ni hofu ya watanzania kwamba, Kama mtu ukimkabidhi Ngariba mtoto;
humfanya anavyotaka, hata mtoto akilalamika kufanyiwa sivyo ndivyo,
huambiwa hatii sheria za Jandoni!
Upo
uwezekano mkubwa na hata Polisi huenda wakaitumia vibaya amri ya Pinda
wakidai, wao ni ndio Afande hakuna kuuliza, na kwa hiyo watawapiga
wananchi ovyo, kwa madai wanatekeleza maagizo, mtu asipotii sheria pasi
shuruti, Pinda aliagiza Piga tumechoshwa!
Utekelezaji
mbaya wa kauli hiyo, itafika mahali utaleta madhara, kwa sababu
wananchi watapigwa na baadaye nao watachoshwa na vipigo vya Polisi, na
kusema inatosha, tumepigwa kiasi cha kutosha, tumeonewa kiasi cha
kutosha, na unyonge wetu ndio uliotufikisha hapo, basi! Enough is
enough.
Baaadhi
ya wasomi wa Uchumi Mzumbe Morogoro walisema, Awali walizoea kusikia
Ugonjwa wa Upofu wa Macho upo Mikoa miwili nchini! Lakini wanadai, sasa
nchi nzima watu watakuwa vipofu, wenye miwani.
Wanadai
sababu kubwa macho ya watoto Shule yataharibiwa kwa mabomu ya machozi,
Maji ya kuwasha na Moshi, kutumika na kuhatarisha afya zao bila sababu
za msingi, ambapo matibu ya uwingi wao, yatayumbisha uchumi kimatibabu.
Waliongeza,
ni kweli akili ni nywele kila mtu ana zake, lakini akili za kuharibu
uchumi kwa mabomu, na baadaye kuanza kuhangaikia tiba ya magonjwa
yatakayosababishwa na vuruguru za tamaa ya baadhi ya watawala
kung’ang’ania madaraka iletayo adha ya kuutweza uchumi, Ipo mlangoni.
nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308
0 Comments