WASANII WATOA MSAADA , WACHEZA NA WATOTO YATIMA TANGA

 Baadhi ya watoto yatima.
 Bob Junior na Nuru
 Msanii Recho akiwa amebeba mtoto pembeni ni  Mkuu wa Wilaya ya Tanga Chiku Galawa.
Recho na Juma Nature.
 Mkuu wa msafara Afisa Uhusiano wa Clouds Media Group ambaye pia anahusika  na Taasisi za Serikali  Vyama vya siasa  na Taasisi za Dindi Simon Simalenga akizungumza na  watoto hao hawapo pichani  mara baada ya kuwasili kituoni hapo aliyeketi kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Halima Dendegu anayefuata ni msanii Recho kulia ni Richie Mavocal na Nuru.
Baadhi ya wasanii wakiwasili katika kituo kimoja cha kulelea watoto yatima Casa Dela Joya  Jijini Tanga hapa walkipokelewa na Mtawa Sofia Loperti.Wasanii hao walikwenda kucheza na kuwaimbia watoto hao mchana kabla ya kufanyika kwa tamasha la Fiesta lililorindima katika uwanja wa Mkwakwani .Pia walitoa zawadi mbalimbali kama vinywaji baridi , unga, biskuti na wengine walitoa fedha kwa baadhi ya watoto walimudu kuimba na kucheza vizuri.


MKUU wa wilaya ya Tanga Halima Dendego ametoa wito kwa wasanii wote wa hapa nchini kuwa na moyo wa kuwakumbuka watoto yatima ambao wanalelewa katika vituo mbalimbali Jijini Tanga.
Dendego aliyasema hayo Jumapili mchana mara baada ya kupokea ugeni wa baadhi ya wasanii waliokwenda  kushiriki katika tamasha la Fiesta lililofanyika katikia  Uwanja wa Mkwakwani tanga.

Wakiwa katika kituo hicho wasanii katika kituo cha Casa Del Joya  Dendego alisema kwamba kwakutokana na kiutendo cha wasanii hao kufika kituono hapo ni moja kati ya faraja ambazo watoto hao wanahitaji kupatiwa na jamii na hasa wasanii ambao wanaishia kuwaona katika luninga tu.

“Unajua hata kama mtu atakuwa anapata kila kitu lakini muziki nao una nafasi yake kwa watoto kama hawa hivyo kufika kwenu hapa hata mimi nimefurahishwa vya kutosha na furaha yangu inakwenda sambamba na watoto hawa si mnaona walivyo furahi hata wao wana vipaji  vya kuimba kama vyenu hebu waoneni walivyo na sura zenye bashasha na furaha” alisema Dendego.

Akitoa historia fupi ya kituo hicho Mtawa Sofia Lo Preto raia wa Italia alisema kituo hicho kilianzishwa 1980 Migoli Mtera mkoani Iringa na baadaye wakahamishia tawi lao jijini Tanga mwaka 2006 pia wanalea watoto 36 ambao 17 wa kiume na 19 wa kike.

Wakati huohuo Afisa Uhusiano wa Clouds Media Group  Limited pia anahusika na Taasisi za Serikali  Vyama vya siasa na Tasisi za dini Simon Simalenga wameguswa kufanya hivyo kwa kuwapeleka wasanii kucheza na watoto kabla ya kufanya onesho lao kwa watu wa kada mbalimbali usiku wa Jumapili.
Tamasha hilo la Fiesta linalofanyika kwa mara ya 11 linatarajiwa kurindima tena Ijumaa katika mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ni Musoma Ijumaa, Shinyanga Jumamosi na Jumapili Jijini Mwanza.

Post a Comment

0 Comments