Hapa akitoka Mahakamani ambapo kesi hiyo imepigwa Kalenda hadi Juni 18 mwaka huu , uchunguzi bado haujakamilika.
(Picha Zote na Francis Dande)
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Kisutu ya jijini Dar es Salaam, jana ililazimika kumwita na kumpandisha kizimbani msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayetuhumiwa kwa kusababisha kifo cha aliyekuwa msanii nyota Steven Charles Kanumba kilichotokea Aprili 7 mwaka huu.
Lulu alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza majira ya 9:02 asubuhi mbele ya hakimu Mkazi Agustina Mmbando ambapo Mwendesha Mashtaka wa Serikali Kenneth Sekwao aliomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa upelelezi wa kesi haujakamilika.

Msanii huyo ambaye anatetewa na mawakili Fulgence Massawe ambaye jana alimwakilisha wakili Kennedy Fungamtama kesi hiyo iliahirishwa kimakosa hadi juni 26 jambo ambalo lilifanya Lulu kurudishwa kizimbani wakati wakijiandaa kuondoka Hakimu alimtaka arudishwe tena kizimbani.
Majira ya saa 9:43 lulu akiwa chini ya ulinzi huku akiongozwa na askari magereza wa kike na wa kiume wasiopungua 15 hyuku msanii huyo akiwa amevalia vazi la buibui jeusi na mtandio mweusi pamoja na raba nyeusi alionekana kushtushwa na kitendo cha kurudishwa tena kizmbani lakini Hakimu Mmbando alimuelewesha kuwa tarehe ya awali ilikosewa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 18 Juni mwaka huu kwa sababu mshitakiwa yupo rumande anapaswa kupandishwa kila baada ya wiki mbili.
Hata hivyo Juni 11 mwaka huu Lulu anatarajiwa kupandishwa tena Mahakama Kuu mbele ya Jaji Fauz Twaib kusikiliza shauri aliloomba kupitia kwa wakili wake la kutaka kutambuliwa kama mkosaji mtoto.
0 Comments