MAREHEMU MZEE KIPARA ENZI ZA UHAI WAKE
Na Mwandishi wetu
ALIYEKUWA Gwiji katika tasnia ya uigizaji hapa nchini, Fundi Said ‘Kipara’ atabaki kukumbukwa kutokana na kuwa jina lake kuwa miongoni mwa majina machache waigizaji wakongwe yaliyopotea..
Marehemu Kipara mwenye umri wa miaka 89 aliyefariki dunia juzi alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya maumivu ya miguu ambapo katika enzi za uhai wake aliuguzwa na wasanii wa kundi la sanaa la Kaole lenye maskani yake jijini Dar es Salaam.
Historia Fupi ya kazi
Alianza sanaa mwaka 1964 kwa kufanya kazi za mitaani, kabla ya kuchukuliwa na Radio Tanzania, Dar es Salaam (RTD) sasa TBC Taifa, akiwa mtangazaji wa michezo ya kuigiza.
Akiwa na katika kituo hicho, aliigiza katika michezo mingi na nafasi zake kubwa zilikuwa zile zenye kuonesha utemi, ambao wengi huita ukorofi.
Ushawishi wa kujikita kwenye sanaa ulitokana na kuwaona wasanii wenzake kama Ibrahim Raha ‘Mzee Jongo’, Hamis Tajiri ‘Mzee Janja’ wote hatunao duniani wakiigiza katika katika kituo cha Redio Tanzania alikokuwa akifanya kazi Kipara.
Akiwa RTD pia alikuwa akifanya kazi ya ulinzi katika Shirika la Reli Tanzania (TRC) jijini Dar es Salaam, ambako alikuwa akifanya kazi kwa ufanisi, kwa sababu alikuwa akifanya kwa muda tofauti.
K wa kukumbushana tu kipindi ambacho alikuwa akishiriki RTD kilikuwa ni kati ya vipindi bora kwa sababu ya kutokana na umahiri wa wasanii wa zamani kama marehemu mzee Jongo na wenzake waliouonyesha, jambo ambalo lilizidi kumpa ushawishika kuingia kwenye sanaa.
Mchezo wake wa kwanza kushiriki uigizaji ulikuwa ni ‘Ahmed Mpiga Kinanda’, uliotungwa na kundi la sanaa la Njoo Uone la jijini Dar es Salaam ambako aliigiza kama kinara katika kutongozaji wanawake na ndiko jina la Kipara lilikoanzia.
Pamoja na ushiriki wake katika mchezo huo pia aliwahi kutunga mchezo wa ‘sitaki’ pasi na kuwa na kundi akiendelea na kazi zake.
Kipara ambaye katika enzi ya uhai wake alishindwa kukumbuka historia yake katika sanaa na kazi ya ulinzi aliyoifanya TRC kutokana na kupoteza kumbukumbu kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua , hiyo ni kwa mujibu wa mwandishi wa makala haya alipofanya mahojiano naye miezi michache nyuma kabla ya mauti kumfika ambapo alisema katika utendaji wake TRC aliwahi kufanya kazi kwa miaka sita na RTD miaka tisa akiwa mtangazaji.
Mwaka 1999, akiwa na wasanii wenzake marehemu Zena Dilip, Tunu Mrisho ‘Mama Haambiliki’, Rasia Makuka, marehemu Rajab Hatia ‘mzee Pwagu’, Fatuma Rajab ‘Kidude’, Chuma Selemani ‘Bi Hindu’ na Madina Hamis ‘Zawadi’ ambao waliunganisha nguvu na kuunda kundi la Kaole wakiongozwa na Mwenyekiti wao Christant Mhenga wa televisheni ya ITV.
Kuundwa kwa kundi hilo ni ushirikiano uliokuwepo baina ya wasanii hao ambao walikutana mara kwa mara ili kuweka sawa mipangilio ya kuandaa michezo mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii.
Pia uanzishwaji wa kundi la Kaole ilikuwa ni kuwa na dira bora ya kuendeleza na kukuza sanaa hapa nchini, hali ambayo iliweza kwa kiasi kikubwa, jambo ambalo lilisababisha kuzaliwa kwa makundi mengi.
Makundi yaliyoasisiwa ni pamoja na kama Kidedea na Mambo Hayo, ambayo nayo yalishika kasi ya juu katika mtandao wa sanaa hapa nchini.
Kipara anasema ameingia kwenye sanaa pasi na kurithi kutoka kwa wazazi wake na kueleza kwamba alivutiwa na kina mzee Pwagu waliokuwa wakiigiza RTD.
Ikumbukwe kuwa pamoja na kuwa muigizaji huyu pia aliwahi kucheza ngoma kwenye kundi la ‘Hiari ya Moyo ’ lililokuwa l ambalo lilikuwa likipiga ngoma ya asili ya Kinyamwezi lililokuwa na maskani yake Ilala, jijini Dar es Salaam.
Asili yake
eneo la Gerezani, Ilala na Kigamboni, lakini asili yake ni Mkoa wa Tabora yaani Mnyamwezi.
Katika familia yao yeye alikuwa mtoto wa nne kuzaliwa kati ya watoto 12 wa mzee Said Kagili wa Mbugani, Tabora. Ameacha watoto saba.
Wito Alioutoa kwa wasanii katika enzi za uhai wake alipokuwa mgonjwaKama tulivyosema hapo juu kwamba Mwandishi wa Makala haya aliwahi kufanya mahojiano na Marehemu Kipara enzi za uhai wake na wakati akiwa mgonjwa na kwa wakati huo alitoa wito kwa wasanii hapa nchini wafanye sanaa ya kweli na wasiipotoshe kwa sababu dira ya maisha ya mwanadamu iko kwenye sanaa.
Alionya wanaotumia sanaa isivyo, walaaniwe na Mungu kwa sababu wanaipotosha jamii.
0 Comments