Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Mkapa akipokea Tuzo yake ya Heshima,
Na Adolph Mapunda
Chama cha waandishi wa Habari nchini (TASWA).Tuzo hizo zilifanyika juzi katika Hoteli ya Movenpick Dar es Salaam na kuratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Serengeti zikihusisha michezo mbalimbali.Rais Mkapa amezawadiwa tuzo hiyo kutokana na mchango mkubwa aliofanya kufanikisha ujenzi wa uwanja wa mpya wa taifa wakati wa uongozi wake.
Kutokana na ushindi huo Mwanaidi amejipatia zawadi ya gari lenye thamani ya shilingi milioni 13 baaya ya kuwashinda wachezaji wenzake Lilian Sylidion wa timu ya Filbert Bayi na Sekela Dominick kutoka JKT Mbeni waliokuwa wakiwania tuzo hizo kwa upande wa netiboli.Mwanaidi ametangazwa kuibuka na ushindi huo baada ya kuidia timu yake ya JKT Mbweni kuibuka na ubingwa wa mashindano ya Ligi daraja la kwanza pamoja na kuisaidia timu ya taifa kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika mwaka jana nchini Singapore.
Wachezaji wengine walioshinda tuzo kwa kufanya vizuri katika michezo yao kwa upande wa soka ni beki wa klabu ya Yanga na timu ya taifa 'Taifa Stars' alipata tuzo za mchezaji bora baada ya kuisaidia timu ya taifa kuchukua ubingwa wa kombe la Chalenji na pia kuiwezesha klabu yake kuchukua ubingwa wa Ligi kuu bara 2010-2011 ambapo kwa upande wa wanawake tuzo hiyo imechukuliwa na Asha Rashidi wa Twiga Stars.Katika mchezo wa kikapu wanaume tuzo imechukuliwa na George Tarimo wa timu ya Savio baada ya kufanya vizuri na kuwa mchezaji bora katika mashindano ya Afrika Mashariki na kati na kwa wanawake Faraja Malaki wa timu ya Jeshi Stars baada ya kuwa mfungaji bora katika mashindano ya majiji.ondia wa ngumi za kulipwa nchini Kalama Nyilawila alipata tuzo baada ya kufanya vizuri katika mapambano ya ndani na ya kimataifa ambapo kwa upande wa ngumi za ridhaa tuzo hiyo imechukuliwa na Selemani Kidunda baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya ubingwa wa taifa na mashindano ya Jumuia ya madola yaliyofanyika mwakajana nchini India na kupata medali ya Shaba.Katima mchezo wa Gofu Hawa Wanyeche aliibuka na ushindi ambapo kwa upande wa wanaume Frank Romani wa klabu Gymkhana Moshi huku katika mchezo wa Cricketi wanaume ni Kassimu Nassoro na wanawake ni Mariamu Saidi ambapo katika mchezo wa Judo tuzo imechukuliwa na Masoud Amour wa Zanzibar.Washindi wengine katika mchezo wa baiskeli ni hamisi Clementi aliyeibuka na ushindi wa kilometa 100 katika mashindano ya Vodacom 2010 na kwa upande wa wanawake ni Sophia Andason aliyeshika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo yaliyofanyika Jijini Mwanza. Grace Hoka Mhariri wa Gazeti la Bingwa wakwanza Kushoto,Khadija aliyesimama na Somoe. Mwanaidi akikabidhiwa tuzo yake ya ushindi na Makamu wa Rais Dk.Gharib Bilal anayeshuhudia ni Waziri wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Dk.Emmanuel Nchimbi.Kwa ushindi huo amepata gaina aina ya Toyota Cresta GX 100, atalalasiku mbili katika hoteli ya Movenpick,Ofa nyingine ni kutoka TANAPA ambako atakwenda kutembelea mbuga za wanyama huku akiwa amelipiwa chakula na malazi. Mchezaji wa mpira wa pete netiball, mwanaidi hapa kabla ya kuibuka mshindi. Kushito ni Asha Mwalala aliyeibuka mshindi wa soka kwa upande wa soka wanawake. Mkurugenzi wa Mahusiano Teddy Hollo Mapunda ambao pia ndiyo wadhamamini wa Tuzo hizo akimkabidhi Tuzo ya Heshima Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Tuzo hiyo imetolewa na TASWA, kutokana na kujali michezo ikiwa ni pamoja na kujenga Uwanja wa Kisasa wa Mpira. Luteni Kanali Mstaafu wa Jeshi pia Mnazi katika soka na Michezo Idd Kipingu.Menyekiti wa TASWA , Juma Pinto akitoa mkono wa pongezi kwa Rais Mstaafu Mkapa. Wakishangilia kwa pamoja, Rai Mastaafu Mkapa, Makamu wa Kwanza Rais Gharib Bilal,Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto na Mkurugenzi wa Uhusiano SBL,Teddy. Khadija katika viwanja vya Hoteli ya Movenpick. Wadau wakiwa kwenye Tuzo hizo. Bendi ta Tanzania House of Talent (THT), wakitoa burudani.
1 Comments