Social Icons

Wednesday, November 3, 2010

ZAWADI ZA MICHUANO YA CECAFA HADHARANI,TENGA:TUNAHITAJI WADHAMINI ZAIDI

Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) jana limetangaza zawadi bingwa wa michuano ya mwaka huu ya Kombe la ‘CECAFA Tusker Challenge’ inayotarajiwa kuanza Novemba 27 hadi Desemba 11, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu Mpya wa SBL Richard Wells alisema bingwa atapata kitita cha dola 30,000 mshindi wa pili dola 20,000 na wa tatu dola za 10,000.

Alisema kuwa zawadi hizo za washindi ni dola 60,000 ambayo ni sehemu ya udhamini wao wa dola 450,000.

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye jana alitangaza ratiba na makundi huku akisisitiza kuwa timu shiriki zipatiwa huduma bora za usafiri wa ndege, chakula na malazi.
Ratiba hiyo ni kama ifuatavyo kwamba mechi zitachezwa mbili kila siku huku muda ukiwa ni saa 8:00 mchana na mechi ya pili itachezwa saa kumi alasiri.

Alisema siku ya ufunguzi mechi ya kwanza itazikutanisha Burundi na Somalia, saa nane mchana wakati mechi ya pili itakuwa kati ya wenyeji Tanzania bara wataokutana na Zambia.

Novemba 28, mechi ya kwanza itakuwa kati ya Sudan na Ethiopia ya pili ikiwa kati ya Rwanda na Ivory Coast.

Novemba 29 Ethiopia itajitupa uwanjani kucheza na Uganda na baadaye Malawi kuikabili Kenya, Novemba 30 Zambia v/s Burundi na Somalia v/s Tanzania Bara.

Desemba Mosi Sudan v/s Rwanda na Ivory Coast v/s Zanzibar.

Desemba 2, Uganda v/s Malawi, Kenya v/s Ethiopia, Desemba 3 Somalia v/s Zambia na Zanzibar v/s Rwanda, Desemba 4 Malawi v/s Ethiopia na Tanzania Bara v/s Burundi.
Wakati Desemba 5 michuano hiyo itaendelea kwa timu ya Ivory Coast Vs Sudan na alasiri Uganda watacheza na Kenya.

Baada ya hapo timu zitapata mapumziko ikiwa tayari zimesha cheza michezo 18 katika makundi matatu ambayo ni Kundi A zimo timu za Tanzania, Zambia, Burundi na Somalia, kundi B – wamo Rwanda, Ivovory Coast, Sudan na Zanziba huku kundi C linazikutanisha timu za Uganda, Kenya, Malawi na Ethiopia.

Baada ya hapo michuano hiyo itaingia katika mzunguko wa pili ambapo itaendelea Desemba 7 huku timu iliyoongoza katika kundi A itakipiga na timu iliyopoteza mchezo huku wakiwa na maksi za juu kushinda wengine.

Mechi nyingine itakayopigwa siku hiyo ni kati ya Mshindi wa kwanza kutoka kundi B atakayecheza na Mshindi wa pili kutoka kundi C.

Desemba 8 mechi itakuwa kati ya Mshindi wa kwanza kutoka kundi C atakayecheza na timu ya iliyopoteza mchezo kwa bahati mbaya.

Mechi ya pili siku hiyo itakuwa kati ya Mshindi wa 2 kutoka kundi A NA MSHINDI WA pili kutoka kundi B.

Siku itakayofuata itawakutanisha mshindi katika mchezo wa 19 na 20 kadhalika siku itakayofuata .

Desemba 11 ni mapumziko huku Desemba 12 ambayo itakuwa siku ya fainali timu iliyopteza mchezo katika mchezo wa 23 na 24 watakutana huku mchana ikiwa ni mechi kati ya mshindi wa 23 na 24.

Aidha mkutano huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Leodgar Tenga na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Serengeti (SBL), Mkurugenzi wa Masoko Carorine Ngungu na Mkurugenzi wa Masuala ya Kampuni (Corporate Affairs) wa SBL Teddy Mapunda.

Musonye amesema timu 12 zimethibitisha kushiriki mashindano hayo ambazo ni wenyeji Tanzania , Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Somalia, Zanzibar, Ethiopia na Sudan.Huku timu alikwa ni Ivoty Coast, Zambia na Malawi.

Naye Mwenyekiti wa CECAFA ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF Leodgar Tenga amesema kuwa wana mpango wa kuendeshaa michuano katuika viwanja viwili huku wakilenga mechi moja ichezwe katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na Dar es Salaam.

Hivyo basi Tenga ametoa wito kwa wadau zaidi kujitokeza ili kutoa udhamini ambapo amebainisha wanahitaji kiasi cha Shilingi Mil.400 .

“Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru SBL kwa kupitia kinywani chake cha Tusker ambao wametoa udhamini wa shil. Milioni 675” ambao utatumika katika malazi, usafiri wa ndani wa timu zote kutoka wanakotoka na kurudi makwao hivyo tunahitaji fedha zaidi ikiwa ni pamoja na huduma za usafiri na malazi” alisema Tenga.

Aliongeza kwa kusema wataomba udhamini kwa Kampuni mbalimbali katika nchi zote ambazo zitashiriki katika michuano hiyo kwa sababu wataweza kujitangaza katika luninga kubwa barani Afrika ya Super Sport.
Nilivutiwa na Vinyago hivi ambavyo vinachongwa na jamaa zetu wa Kimakonde.
Saidi makala Mwandishi wa gazeti la Micheezo na Burudani la Bingwa naye hakutaka kupitwa anayefuata chini ni Wilbert Moland kutoka gazeti la wiki la Champion akiwa katika pozi ndani ya hoteli ya New Afrika leo.

Majuto Omary wa gazeti la kizungu la The Citizen ambaye pia ni mchezaji wa kutumainiwa katika timu ya waandishi ya TASWA FC yeye hakuvutiwa na vinyago wala nini alijimwaga hapa akituangalia tu shobo zetu.
Kambi Mbwana Mwandishi Gazeti la Mtanzania naye aliguswa na mapambo haya pale New Africa Hotel.
Wanablog wanapokutana katika maeneo ya kazi kushoto ni mimi na Papaa Bukuku a.k.a. mzee wa http://www.fullshangwe.blogspot.com/
Mashostito wa 'longtime ago' ghafla tukakutana katika mitaa ya Samora Jijini Dar es Salaam baada ya kupotezana kwa muda mrefu Kulia ni Talle a.k.a.Tally Kassim ni mjasiriamali na anamiliki Tailoring Mart yake Mitaa ya Kinondoni kaa tayari kupata na kuona ubunifu wake ambapo alionyesha cheche zake katika shindano la kumsaka Miss Kinondoni 2010.

1 comment:

Unknown said...

Mashostito mmependeza. Khadija blog yako umeirekebisha vizuri saaana, mimependa. Kazi nzuri. Tally Kassim mbona amejificha sana, ndugu yangu? Ukimuona tena mpe salam. Nasubiri kwa hamu kuona ubunifu, hongereni sana kwa kazi nzuri.

 
 
Blogger Templates