Social Icons

Wednesday, November 3, 2010

TATHMINI YA CCM KUHUSU UCHAGUZI HII HAPA

Meneja wa Kampeni za CCM, Abdulrahman Kinana amezungumza na kutoa tathmini ya chama hicho kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 31 Oktoba 2010. Kinana amesema kuwa wapinzani wa CCM wamefanikiwa kupata jumla ya majimbo 51 ambapo majimbo 29 yamenyakuliwa na upinzani Tanzania Bara il hali majimbo 22 yamemilikiwa na upinzani huko Zanzibar (18 Pemba na 4 Unguja). Ikilinganishwa na uchaguzi uliokwisha 2005, ambapop upinzani Bara walipata viti 6 pekee na Zanzibar viti 19, mwaka huu 2010 wapinzani wamefanikiwa kunyakua majimbo mengi zaidi (23 Bara, 3 Zanzibar). Kinana amesema ongezeko hilo linatokana na kukua kwa demokrasia na vile vile akagusia kuwa, huenda hatua za CCM za kukemea vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watu walioonesha nia ya kuwania nyadhifa za uwakilishi kupitia chama hicho, kilichochea kuundwa kwa makundi, jambo ambalo huenda likawa limechangia kwa wao kuanguka katika baadhi ya majimbo. Akasema vile vile kuwa MwanaCCM yeyote ambaye anadhani hakutendewa haki katika matokeo ya uchaguzi huu na akataka msaada, basi CCM itakuwa tayari kumsaidia. Amemaliza kwa kuwapongeza Wazanzibari kwa mwenendo mzima wa uchaguzi na kwa ushindi walioupata.

No comments:

 
 
Blogger Templates