WABUNIFU 24 KUCHUANA WIKI YA MITINDO YA KISWAHILI

Wabunifu 24 toka nchi zinazoongea lugha ya Kiswahili wanatarajiwa kuonyesha kazi zao katika maonyesho ya tatu ya ‘Swahili Fashion Week’ ambayo kwa mwaka huu yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 4 hadi 6.

Maonyesho hayo yenye lengo la kuwaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maeneo hayo, kwa mara ya kwanza kutakuwa na maonesho ya bidhaa mbalimbali.
Mwandaaji wa maonyesho hayo, Mustafa Hassanali anasema kwamaba p
moja na maonyesho ya mavazi, mwaka huu Swahili Fashion Week itakwenda sambamba na tamasha la maonyesho ya bidhaa mbalimbali zenye asili ya mswahili kutoka mwambao wa Afrika mashariki.

Anasema wanafungua milango zaidi kwa ajili ya watazamaji wapya wa Swahili Fashion Week, ambao watapata fursa ya kununua bidhaa mbalimbali katika tamasha hilo ambalo pia litahamasisha ubunifu zaidi katika bidhaa zinazokwenda sambamba na maisha halisi ya jamii ya watu wanaoongea lugha ya Kiswahili kwa kukutana pamoja na kubadilisha mawazo na kujifunza uzoefu mpya katika masuala yanayohusiana na sanaa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments