WASHIRIKI 16 wamejitokeza kushiriki katika shindano la mwaka huu la kumsaka Kimwana wa Twanga Pepeta 2011. Kwa mujibu wa Mratibu wa shindano hilo Maimatha Jesse amesema washiriki wote ni wakazi wa Jiji la Dar es salaam kutoka katika wilaya zote. Shindano hilo ambalo litakuwa likifanyika kwa mara ya tatu sasa huku likiandaliwa na Kampuni mbili ambazo ni ASET na MANYWELE Entertainment wote kwa pamoja wametoa wito kwa kina dada kujitokeza kwa wingi zaidi kwani nafasi bado zipo. Katika mkutano wake wa awali Mratibu Maimatha ‘Mai’ alitangaza zawadi kwa mshindi wa kwanza kuwa atapatiwa duka la vipodozi lenye bidhaa za thamani ya Shilingi Mil.5 huku likiwa limelipiwa kodi kwa muda wa miezi sita tu. Mai alisema baadae wiki hii washiriki wote wataanza rasmi mazoezi ya kucheza katika miondoko ya bendi ya Twanga Pepeta kwa ajili ya utambulisho uliopangwa kufanyika Mei 6 kwenye Club ya Sun Siro uliopo Sinza Dar es Salaam. Katika utambulisho huo bendi ya Twanga Pepeta watasindikiza sambamba na msanii aliyetia for a kwenye tunzo za muziki za mwaka 2010 , 20% . Wadhamini wa shindano la Manywele Kimwana wa Twanga Pepeta 2011 ni pamoja na East Africa TV&Radio, Sinza BM Barber shop.
NFRA SONGEA YANUNUA TANI ZAIDI YA 72,000 ZA MAHINDI MKOANI RUVUMA
-
Na Mwandishi Wetu,Ruvuma
WAKALA wa Taifa wa hifadhi ya chakula(NFRA)Kanda ya Songea mkoani
Ruvuma,imenunua tani zaidi ya 72,000 za mahindi kutoka kwa ...
4 hours ago
0 Comments