Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi Kata ya Viziwaziwa ambacho kimeanza 2023 kwa nguvu za wananchi wa Kata hiyo pamoja na wadau wa maendeleo.Amesema, kwa wakati mwingine wananchi wamekuwa wanaibua miradi, na kisha serikali inakuja kumalizia miradi hiyo.na katika ujenzi wa Kituo hicho wananchi wamechanga takribani kiasi cha milioni 12 na bado wanaendelea kuchanga.
Naye, Diwani wa Kata ya Viziwaziwa Mhe. Mohamedi Chamba ameishukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuboresha maisha ya watanzania na kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali, pia amemshukuru Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Mhe. Dkt Nicas Mawazo kwa kuchangia mabati 500 kwa ajili ya kupaua Kituo hicho cha Polisi.
Aidha amemshukuru Mbunge wa Jimbo Mhe. Silyvestry Koka na kuwaomba wadau wa maendeleo waendelee kuunga mkono juhudi za serikali ili kufanikisha kumaliza ujenzi wa kituo hicho cha Polisi.
Katika harambee hiyo, Waheshimiwa madiwani kutoka Kata ya Misugusugu Mhe. Ally Mwinyi Simba na Diwani Kata ya Visiga Mhe. Saidi Mpaki waliweza kufika na kushiriki hafla hito na kuahidi watahakikisha kituo hicho kinamalizika ndani ya muda aliosema Mstahiki Meya kwa kuwaleta wadau wa maendeleo kuweza kuchangia.
Baadhi ya wananchi wa Kata hiyo wamefurahj kuona kero yao ya muda mrefu ya kutokuwa na kituo cha Polisi inaenda kuisha, wamempongeza Mstahiki Meya kwa moyo aliouonesha wa kufanya harambee na kupatikana kwa kiasi cha Tsh 900,000 , tofali 750 na mifuko ya saruji 10.

0 Comments