WAJUMBE WA BODI YA ZABUNI NGORONGORO WATAKIWA KUSIMAMIA MPANGO MKAKATI WA SHIRIKA

 

Wajumbe wa Bodi ya zabuni ya Mamlaka ya Hifadhi ya *Ngorongoro* wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuoanisha na mpango mkakati mpya wa miaka mitano wa mamlaka hiyo ulioanza kutekelezwa hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia rasilimali watu na utawala *Salma Chissonga* ametoa kauli hiyo katika kikao cha kawaida cha Bodi ya zabuni kinachoendelea Jijini Mwanza.

*Chissonga* amesema kuwa mahitaji yote ya manunuzi ya Mamlaka lazima iangalie mipango ya taasisi kupitia mpango wa miaka mitano sambamba na kusimamia thamani ya fedha ya kila mradi unaofanyiwa manunuzi

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kinatarajia pia kupitia miongozo mbalimbali ya manunuzi inayotolewa na Serikali yenye lengo la kuhakikisha watanzania pia wananufaika na manunuzi ya umma.

Post a Comment

0 Comments