Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utali imeipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa kuimarisha uhusiano na wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi na kuitaka kuendelea kushirikiana na jamii ya wananchi hao.
Akizungumza kwa niaba ya wabunge wa kamati hiyo Mwenyekiti wa kamati mhe. Timotheo Mnzava amesema Kamati inaridhishwa na hatua hizo ambazo zinaonesha mustakabali mwema wa uhusiano wa wananchi na mamlaka hasa utekelezaji wa huduma za kijamii.
Kamati hiyo imeenda mbali kwa kuridhishwa na mageuzi mbalimbali ya kimfumo hasa matumizi ya teknolojia, miundombinu ya barabara na jitihada kubwa za kutangaza utalii katika ngazi za kitaifa na kimataifa kidijitali.
Kamati hiyo imeenda mbali kwa kuridhishwa na mageuzi mbalimbali ya kimfumo hasa matumizi ya teknolojia, miundombinu ya barabara na jitihada kubwa za kutangaza utalii katika ngazi za kitaifa na kimataifa kidijitali.
Akielezea utendaji kazi wa mamlaka hiyo Kamishna wa Uhifadhi Abdul-Razaq Badru amesema Ngorongoro inafanya jitihada kubwa kusimamia ujenzi wa barabara ya kutoka geti la Loduare-Golini ambapo ujenzi wa kipande cha kwanza cha km 29.5 cha Loduare -Seneto unaendelea..
Ameongeza mamlaka imepiga hatua kubwa katika matumizi ya mfumo wa kisasa wa vipenyo ambao unawawezesha wageni kutumia muda mfupi kuingia na kutoka ndani ya hifadhi.
Waziri wa Maliasili na Utalii mhe. Dkt.Ashatu Kijaji aliishukuru kamati hiyo kutokana na ushauri,maelekezo na usimamizi wake kwa wizara hiyo na taasisi zake.



0 Comments