Na Clemence Kagaruki
Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu Chana Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Kibaha Mjini ikiongozwa na Mwenyekiti Mwl. Mwajuma Nyamka imeendelea na ziara ya kukagua Miradi ya maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 Kwa kipindi cha miezi sitaJulai - Desemba 2024.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi imenufaika na mradi wa maji wa kisima kirefu cha maji wenye thamani ya Shilingi Mil.45 900,000 kutoka Taasisi ya DirectI Aid Society.
Mradi huu ulianza tarehe 10 Julai 2024 na kumalizika tarehe 12 Agosti 2024, lengo la mradi huu ulikuwa na lengo la kuondoa changamoto ya upungufu ya maji iliyokuwepo kutokana na kutegemea chanzo kimoja cha maji (DAWASA).
Mradi huu unatumia nishati za uhakika Umeme kutoka TANESCO, Umeme wa jua na 'Standby Generetor'.
Pampu inazalisha kiasi cha lita 10000 kwa saa moja hii imepelekea kumalizika kabisa changamoto ya maji ambayo matumizi yanakadiriwa kuwa lita 10000 kwa siku .
Kwa heshima kubwa tunaipongeza serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kujenga ushirikiano na Taasisi mbalimbali zenye mitazamo na malengo chanya ya kusaidia jamii zenye uhitaji kwa sasa wafanyakazi na wagonjwa wa ndani 920 kwa siku hospitalini hapo wana uhakika wa kupatikana huduma ya maji kwa kipindi chote cha mwaka.
Idaa ya Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Wilaya Kibaha Mjini.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon akizungumza na Mwenyekiti wa Wanawake Wilaya ya Kibaha Mwl.Mwajuma Nyamka ambaye ameongoza Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye ziara ya kukagua miradi.


0 Comments