MAHUNDI AMFARIJI MWENYEKITI UWT TAIFA MARY CHATANDA KUFIWA NA DADA YAKE JIJINI MBEYA

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amefika kutoa pole kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Taifa (UWT) Mhe. Mary Pius Chatanda aliyefiwa na dada yake marehemu Losca Mwakyoma Mtaa wa Mwantegule Kata ya Isyesye Jijini Mbeya.


Mazishi yamefanyika Machi 1,2025 katika makaburi ya Isyesye na kuhudhuriwa na Viongozi wa UWT Taifa akiwemo Makamu Mwenyekiti Zainabu Shomari,Riziki Kingwande Naibu Katibu Mkuu Taifa na Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson.

Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amefika msibani muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea Zimbabwe kuiwakilisha nchi katika mkutano wa Kimataifa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara

Post a Comment

0 Comments