𝐌𝐇𝐄 𝐌𝐇𝐀𝐍𝐃𝐈𝐒𝐈 𝐌𝐀𝐑𝐘𝐏𝐑𝐈𝐒𝐂𝐀 𝐌𝐀𝐇𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐀𝐇𝐔𝐃𝐇𝐔𝐑𝐈𝐀 𝐔𝐙𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐍𝐁𝐂 𝐊𝐈𝐆𝐀𝐍𝐉𝐀𝐍𝐈 .

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amehudhuria hafla ya uzinduzi wa utoaji huduma kidijitali katika Benki ya Taifa ya Biashara(NBC) Jijini Dar es Salaam mgeni rasmi akiwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa .

Katika hotuba yake Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameishukuru Benki ya NBC kwa namna ilivyochukua hatua ya maendeleo kidijitali hivyo kuiunga mkono Serikali sanjari kukuza uchumi jumuishi ndani na nje ya nchi.

Aidha Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inatambua jitihada kubwa zinazofanywa na Benki ya NBC kuhakikisha inatoa huduma bora na za haraka kwa wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan alipanua wigo kwa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Ili kuongeza ufanisi kibiahara kwa njia ya kidijitali Kitaifa na Kimataifa kwa kutumia mkongo wa Taifa utakaofikiwa na mikoa yote nchini.

Post a Comment

0 Comments