TANZIA
Mwanamuziki nguli mwenye asili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Kikumbi Mwanza Mpango King Kiki (77) aliyefariki usiku wa kuamkia leo, atazikwa Jumatatu Novemba 18.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu Jose Kikii amesema hayo leo Novemba 15 alipozungumza na waandishi wa habari kuwa heshima za mwisho kwa marehemu baba yake zitaolewa Uwanja wa Leaders Club na baadaye atazikwa makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Msiba wa King Kikii upo nyumbani kwake Mtoni kwa Aziz Ali Temeke.
0 Comments