*MTV kuachia filamu yake mpya
NEW YORK, Marekani
IKIWA imetimia miaka 10 tangu kutokea kifo cha mwimbaji maarufu wa R&B, duniani Aaliyah Dana Haughton ‘Aaliyah’ Televisheni ya MTV inatarajia kumkumbuka kwa kutoa filamu yake inayokwenda kwa jina la ‘The Aaliyah Movie’ iliyoongozwa na Bill Condon, huku mwigizaji Keisha Chante anatarajiwa kuigiza kama Aaliyah. Kifo chake
Mwanadada huyo aliyezaliwa Januari 16, 1979 alifariki Agosti 25, 2001 na watu wengine nane kwa ajali ya ndege iliyotokea Bahamas wakati wakiwa wanapiga picha za video za wimbo wake wa ‘Rock the Boat’.
Katika taarifa iliyotolewa kuhusu ajali hiyo ilieleza kuwa rubani, Luis Morales III, alikuwa amelewa pombe na kuvuta dawa za kulevya huku akiwa ameendesha bila leseni.'
Historia
Mwimbaji huyo mwenye vipaji lukuki ikiwamo uigizaji na uanamitindo amezaliwa mjini Brooklyn, New York na kukulia Detroit, Michigan.Akiwa katika umri wa miaka 10, alianza kuonekana katika vipindi vya kuwasaka nyota waimbaji ikiwa ni pamoja na kupiga shoo na mwimbaji Gladys Knight.Alipofikisha miaka 12, nyota ya Aaliyah ilianza kung’aa na kupata dili la kufanyakazi na Studio za Jive Records akiwa na mjomba wake Barry Hankerson. Mjomba wake Hankerson ndiye alimtambulisha kwa mwimbaji R. Kelly, ambaye alikuja kuwa mshauri wake katika masuala ya uandishi wa nyimbo na utayarishaji way albamu yake ya kwanza ya ‘Age Ain't Nothing but a Number’ albamu iyopata mafanikio na kuuza jumla ya nakala milioni tatu kwa Marekani. Baada ya kuachia albamu hiyo ya Age Ain't Nothing but a Number kulitokea maneno yaliyokuwa yakihusisha kuhusu mahusiano yao na R. Kelly ambao walidaiwa kuoana kwa siri wakati huo akiwa katika umri wa miaka 15 ndipo akautoa kama dongo kwa wale wanaosema. Kutokana na kufanyiwa msaada huo ulisabisha R.Kelly, kuhusishwa na kufanya mapenzi na Aaliyah ambaye kwa wakati huo alikuwa mdogo hajafikisha miaka 18 ya watu wazima. Uwezo wake ulimfanya aweze kufanya kazi na waandaaji wakubwa kama vile Timbaland na Missy Elliott katika albamu yake ya pili ‘One in a Million’ ikiwa imeuza nakala milioni 3.7 kwa Marekani pekee ikiwa imeuza jumla ya nakala milioni nane duniani.Mwaka 2000, Aaliyah alionekana katika filamu yake mpya inayojulikana kama ‘Romeo Must Die’ ambayo aliitolea wimbo unaokwenda kwa jina la "Try Again" ambao nao ulifanikiwa kufanya vema katika chati mbalimbali na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika nafasi 100 za Billboard na kutwaa tuzo za Grammy kama mwimbaji bora wa kike.Baada ya kuachia filamu yake ya Romeo Must Die, alishiriki kucheza filamu nyingine ya ‘Queen of the Damned’. Filamu hizo zilizomsaidia kupata utajiri unaofikia dola milioni 18.6 kwa wiki moja ya kwanza.Filamu hiyo ilifanikiwa kupata tuzo ya video ya mwimbaji bora wa kike na filamu bora ya mwaka 2000 ya MTV. Baada ya wiki moja ya kufariki kwake studio ilitoa filamu iliyokwenda kwa jina la ‘Rock the Boat’.Baada ya kutoka kwa kazi hizo alifanikiwa kujikusanyia utajiri uliofikia kiasi cha dola milioni 15.2 kwa wiki moja pekee.
Hayati Aaaliyah enzi za uhai wake.
0 Comments