KURUI Vs KISARAWE WAKIPIGA MZENGA


Mzenga,Kisarawe 

Timu za soka Kata ya  Kisarawe na Kurui jana tarehe 17 Januari   2025 zimetoka sare ya goli moja moja ikiwa ni katika hatua ya kuwania kucheza  mechi ya fainali ya michuano ya Jafo Cup itakayochezwa Februari 2 ,2025.

Wakizungumza mara baada ya kumalizika  kwa mechi hiyo ambayo wachezaji wa timu zote  wameonesha uwezo wa hali ya juu kwa kusakakata kabubu yenye viwango kwenye mechi iliyochezwa katika  Uwanja Mzenga Wilayani  Kisarawe Mkaoni Pwani jana jioni tarehe 18 Januari  2025.

Akizungumza  mara baada ya kumalizika  mechi hiyo Kapteni wa timu ya Kisarawe  Jonathan Mabuya amesema kuwa  anamshukuru  mungu  mchezo mzuri na kusisitiza  kuwa matokeoni matatu kushindwa kutoa sare na kutolewa .

"Mchezo wa leo umeshapita  tunawaahidi mashabiki wetu wa Kisarawe  kuwa kwenye mechi ya marudiano  tutashinda" amesema Mabuya.

Kapteni wa timu ya Kurui   yenye maskani yake Kata ya Mzenga   amesema  Kisarawe wajiandae watakapokutana kwenye mechi ya marudiano  sababu lengo lao ni kucheza fainali  na si vinginevyo.

Diwani wa Kurui  Mhe.Mussa Ruhikuni amesema kuwa michuano hii inakuza  uhusiano  miongoni mwa Kata za Kisarawe  pia  kwa niaba ya wananchi  anamshukuru  Mhe.Waziri  wa Viwanda na Biashara Dkt.Selemani Jafo  ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kisarawe  kwa kupitia michuano  ya Jafo Cup vijana  wameepukana na kujiunga na makundi yasiyofaa.
Diwani wa Kata ya Kisarawe Abel Mudo akikagua timu ya Kirui  inayoshiriki  michuano  ya Jafo Cup  yenye maskani Mzenga ambao ndiyo walikua wenyeji  wa mechi hiyo.
Aidha Diwani wa  Kata ya Kisarawe  Abel  Mudo amesema kuwa  michuano hii inaleta burudani  huku amesifu mechi ilivyokua ya kuvutia  kwa sababu timu zote zinaonekana zimejiandaa vya kutosha .

"Nawapongeza waandaaji wa Jafo Cup  kwa sababu wananchi  wetu wamefurahia na kujitokeza kwa wingi kushuhudia  mtanange huu pongezi kwa Mh.Jafo kwa kuja na wazo hili la kuwakutanisha vijana  wa rika  zote michuano  hii iendelee" amesema Mh.Diwani Abel.

Kocha wa timu ya Kisarawe  Maliki Hilali  Dachi amewaahidi ushindi  wa kishindo  mashabiki wa Kisarawe FC  kwenye  mechi yao ya marudiano  na kusisi ushindi utakuwa kwao na watabana ipasavyo Kurui FC.
Kocha wa Kurui FC Fikiri Kikondo amesema kuwa wao hawajawahi kushindwa kwenye michezo yote ya nyumbani na ugenini hivyo Kisarawe FC wajipange tena watakapokutana nao Januari 25  mwaka huu
Michuano ya Jafo Cup imeanza Juni   2024  imeshirikisha  timu kutoka Kata zote 17 na  Vijiji 65  
Mshindi wa Jafo Cup ataondoka na done nono  kiasi cha Mil.2 pamoja na pikipiki mbili huku mshindi wa pili ataondoka na Mil.1 pamoja na pikipiki fainali hiyo itachezwa   Manerumango  Kisarawe  Pwani.

Post a Comment

0 Comments