Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe. Caroline Kitana Chipeta akiwa kavalia mavazi ya asili ya mwanamke wa kimwambao kwenye Tamasha la Mabalozi 2024 (Embassy Festival) nchini Uholanzi lililovutia watazamaji zaidi ya 50,000 mjini The Hague.
Na Mwandishi Maalumu
Ubalozi wa Tanzania umetia fora kwenye Tamasha la Mabalozi 2024 (Embassy Festival) nchini Uholanzi lililovutia watazamaji zaidi ya 50,000 wikiendi iliyopita mjini The Hague.
Idadi hiyo ya wahudhuriaji nkatika Tamasha hilo ni pamoja na makumi ya wana Diaspora wa Tanzania waishio nchini humo pamoja na wawekezaji wakubwa kutoka Tanzania kama vile PetroBas NL.
“Tamasha hilo ni fursa ya kipekee kuonyesha utajiri wa utamaduni wa Tanzania, nasi nafasi hiyo hatukuipoteza hata kidogo,” Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe.Caroline Kitana Chipeta amesema.
Balozi Chipeta amesema fursa zilizojitokeza kwenya tamasha hilo ni kuanzia kukuza utalii na lugha ya Kiswahili hadi mchanganyiko wa mitindo ya zamani na ya kisasa, ambapo Tanzania iliibuka kuwa kivutio kikubwa.
Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe. Caroline Kitana Chipeta akipongezwea na Meya wa Mji wa The Hague kwa Tanzania kuwa kivutio kikubwa kwenye Tamasha la Mabalozi 2024 (Embassy Festival) nchini Uholanzi lililovutia watazamaji zaidi ya 50,000 mjini The Hague.
0 Comments