Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Fatuma Mganga amesema tunafahamu suala la kilimo huwezi kulitenganisha na TARI na huwezi ukatengamisha uchumi wa nchi yetu na kilimo.
RAS Mganga amesema hayo alipokuwa mgeni rasmi siku ya korosho wakati wa maonesho ya wakulima nanenane Kitaifa Jiji Dodoma pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya TARI.
Amesema kwa sababu karibu yetu wananchi wengi waanjishughulisha na kilimo na tunapoongelea kilimo wakati huu tunaongelea kilimo biashara.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Hamidu Mbwana amesema kilimo cha korosho kimetuletea tija sana kwenye upande wa uzalishaji kutoka tani 210,000 msimu wa 2021 -22 mpaka msimu wa 2025-26 tumeweza kuzalisha tani 618,000 tukiwa na lengo la kuzalisha tani Mil.1 ifikapo 2030.
Kwa sababu ya mafanikio tuliyopata upande wa uzalishaji tumeamua kuongeza thamani ya zao hili na kimsingi pamoja na kwamba zao hili linaleta tija sana kwa kuongeza pato kwa wakulima na kuongeza mapato kwa serikali .
Mkurugenzi Mkuu wa TARI Dkt.Thomas Bwana amesema Dira 2050 inataka tufikie uchumi wa mkubwa wa juu katika uchumi hatuwezi fikia huko bila nchi kukua sisi tunategemea ongezeko la tija hili litaongezeka tu kama tutatumia teknolojia sahihi zinatoka wapi zinatoka kwenye tafiti kwa hiyo ukiangalia utafiti ndiyo roho ya Dira.

0 Comments