TWANGA WALIVYOTWANGA 'TWANGA CITY' USIKU WA JANA

Bendi ya Muziki wa dansi ya The African Stars International wafunika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mago Garden 'Twanga City' Kinondoni Jijini Dar es Salaam. leo mchana wako Mbalamwezi ambako watashirikiana na msanii Dully Sykes wakati usiku watakuwa TCC Chang'ombe.
Hapa sijui nikwambie nini huyu dada anaonekana jinsi mzuka ulivyompanda.
Hapa waimbaji wa bendi nao wakionyesha shoo sambamba na wachezaji wa kiume.

Hapa shoo ikiendelea kutoka kushoto ni Kimobitel, Super K na Janet.

Dogo Rama mwana Kigoma akiwa jukwaani usiku wa jana.

Muumini alipokuwa jukwaani aah bwanaa alikusanya kodi ile mbayaaa yaani wadaiwa walijipeleka wenyewee bila kuitwa hakika Muumini hivi sasa yuko juu na amerudi katika chati na anapendwa na mashabiki wengi.

Kiongozi wa bendi ya Twanga Luiza Mbutu akitabasamu mara baada ya kumwona shosti Bongoweekend ndani ya nyumba ikiwa ni baada ya kuwamiss sana kutokana na majukumu ya kuwa mikoani kikazi zaidi hasa kila wikiendi.

Maua ya Twanga kushoto Janet na Luiza .

Huyu muimbaji ni zao la Muumini Mwinjuma achana nae akiwa jukwaani lazima sauti yake ikupenye.

Shoo ikiendelea huku kiongozi wa bendi hiyo Luiza Mbutu 'Mama B' akiwakilisha.

Muimbaji kiraka Charls Baba Mwana Tanga hapa ni kama kawa kama dawa enh.

God Kanuti mkung'uta gitaa aliyekataa mijihelaa kutoka bendi moja siitaji jina mkanipa hila buree hapa akiendeleza kulitwanga Twanga.

Mwanadada Janet Isinika 'Mama Yoko' akiwa jukwanii na miondoko mipya ya Twanga.

Mimi na Kambi Mbwana kutoka gazeti la Bingwa sebene likatunogea full kujiachia nasisi tukasebeneka Chezea Twanga weweee shaurilooo.

Mpiga ngoma Kaposhoo mtoto wa Kiha aliyekwambia ukiwa mlemavu wa viungo halafu usifanye kazi nani huyu ni mlemavu wa miguu lakini anapiga mzigo ile mbaya kaa tayari nitafanya nae mahojiano soon na yeye ameahidi kutomboka ile mbayaa.

Hapa nikiingia kwenye ukumbi wa Mango Garden Kinondoni usiku wa jana kuamkia leo.

Muimbaji wa kike kati ya waimbaji watatu wa bendi ya Khadija Mnoga 'Kimobitel' akiwa jukwaani.


Lilian Tungaraza 'Internet' hapa akiwa full mzukaaa.

Post a Comment

6 Comments

Anonymous said…
Picha nzuri sana na matukio mazuri. lakini wacha ubaguzi maana jijini dar kuna band nyingi. Tuletee ladha tofauti na hii ya twanga angalau tujue uko fare sweetie!
Anonymous said…
Na kweli mdau hapo juu umenena,blog hii kila mara hutoa habari za Twanga tu
nilidhani ni mimi tu ninaeliona jambo hili,Kusema ukweli kama wewe ni muandisha wa habari uliyekomaa au kutimia vizuri katika fani hii si vizuri habari zako zilalie upande mmoja tu,hali hii inatufanya tuwe bored,kuna mdau mmoja aliwahi kumuuliza mwana blog huyu kama yeye huwa anapata posho au ana fungu Twanga,maana dalili zinaonekana.Jitahidi kubadili tabia ili blog yako iende na wakati,siyo kila siku Twanga,tunataka tuone sehemu za burudani zingine na pia bendi mbali mbali,rekebisha hili tafadhali.
Anonymous said…
Kwa mtazamo wangu naona ni kama blog hii inamilikiwa na Twanga,maana tukija kenye swala la burudani ni Twanga tu,yaani kila siku.Ingefaa basi Twanga waanzishe blog yao kama bendi zingine kuliko kutegemea blog hii,Hakuna jipya tunaloliona isipokuwa Twanga kila waendapo,inachosha kama walivyosema wadau hapo juu,tunapenda kuona habari kutoka kwenye clubs zingine na pia kama ni bendi bendi zingine maana bendi zipo nyingi Dar na siyo Twanga tu,Ila kama una posho unapokea huko
hatuwezi kuingilia maslahi yako,ila jitahidi kuwa "NEUTRAL"
Mdau Johanessburg-S.Africa.
Anonymous said…
kwani kuna tatizo gani mtu kupenda kitu cha aina moja, jamani muacheni huyu dada afanye anavyojiskia kama anawakera kuweka post za Twanga si muingie katika blog wanazoweza bendi mnazozipenda?kama vipoi fungueni na ninyi za kwenu
Anonymous said…
MIJITU MINGINE BWANA HOVYOOOO MUMMY ACHANA NAO HAO MAMLUKI INAWAUMA NA KUSHABIKI NA MIBAND YAO Iliyojaa uswahili kazi kutumbuiza viti badala ya watu haloooo tupe mambo mama , kama mnaumia fungueni za kwenu tuachieni sisi na blog yetu pendwa
Anonymous said…
Msimpe kichwa huyu dada blog ni sehenu ua ni uandushi wa habari na si Ushabiki, sasa huyu dada anaonekana ni shabiki na anajipendekeza sana Twanga,Siyo blog yake hii tu,hata nyinginezo zikiwa kila siku zinatoa utumbo huo huo basi sisi kama wasomaji hukacha.Inapendeza kama ukifungua blog unakuta habari mpya na pia picha mpya siyo habari hizo hizo na picha hizo hizo !!hapa mimi nawasapoti hao wadau juu blog hii iache kujipendekeza kwa Twanga,maana tunaliona hili wazi wazi.Mwandishi wa habari aliyekomaa ktk fani hii huwa haitakikani aonyeshe ushabiki wa timu,bendi au kikundi chochote,hapo ndipo atakubalika hata kimataifa,na siyo kuwa mwana blog wa vichochoroni ,la sivyo blog itabaki kuwa "LOCAL!MWANDISHI BADILIKA.