TUVUMILIANE NA KUHESHIMIANA KAMA WATANZANIA - DKT. BITEKO

Mamia ya Wakatoliki Wamiminika Uwanja wa Uhuru Kongamano la Ekaristi Takatifu

 Watanzania Wahimizwa Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewaasa Watanzania kuishi kwa kuvumiliana, kuheshimiana na kupendana kama ilivyoagizwa na vitabu vya Mungu.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Septemba 15, 2024 katika Kongamano la Tano la Ekaristi Takatifu Kitaifa lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaaam.

“ Wote tuliokuja hapa tumesikia mahubiri mazuri, tumehubiriwa kuwa wamoja zaidi tukavimiliane zaidi  na kuheshimiana kama Watanzania wamoja. Kuwa na mawazo tofauti  kusitufanye  tugawanyike Ekaristi Takatifu  hii itufanye tuwe wamoja,” amesema Dkt. Biteko.

Amesisitiza “ Tuwafundishe jamii tuliyonayo kuwa na huruma kwa watu wote wanaohitaji na muhimu zaidi kuwa na huruma na taifa letu la Tanzania.”

Akizungumzia kaulimbiu ya Kongamano hilo inayosema “Udugu Kuponya Ulimwengu, Ninyi Nyote ni Ndugu”, Dkt. Biteko amesema kuwa kauli mbiu hiyo ni muhimu na inawaunganisha watu pamoja.

Vatican nchini Tanzania Askofu Mkuu Angelo Accattino amesema kuwa Kongamano hilo limeeleza umuhimu wa Ekaristi Takatifu kama kiini cha imani yao.

“Ekaristi inatuunganisha na kristo na ndugu zetu katika imani Ekaristi ina imarisha upendo wetu kwa Mungu. Naipongeza Serikali kwa kufanya matukio kama haya kwa uhuru na amani” Amesema Askofu Accattino.

Kongamano hilo limekonga nyoyo za maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki kutoka maeneno mbalimbali nchi nzima limehudhuriwa na mamia ya viongozi wa dini wakiwemo maaskofu, mapadre na watawa.

Ambalo limehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Albert Chalamila.

Viongozi wengine ni Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emannuel Nchimbi na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika.

Post a Comment

0 Comments