Tunawahimiza wadau kutengeneza bidhaa wanazozizalisha kwa kutumia.maligjafi ya Mkonge kama Gypsum kwa sababu kuu inatunza mazingira tofauti na za sasa ambazo zinatumia manila (plastic).Pia tunahimiza wawekezaji kote nchini waongeze matumizi ya Mkonge kwani linaweza likatoa bidhaa nyingi ikiwemo kurina asali na kutengeneza sukari kwa kupitia tunda lake ambalo linafanana na nanasi wenzetu katika nchi ya Mexico na Afrika Kusini wanazalisha asali na sukari kupitia tuna hilo.
Akizungumza katika maonesho ya nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Dkt .John Samuel Malecela Nzuguni Jijini Dodoma Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya Mkonge Bodi ya Mkonge Tanzania Simon Kibasa amsema mkonge ni zao la biashara la muda mrefu zao hili liliongizwa na wajerumani 1893 likitokea Mexico na Ujerumani likaletwa Tanganyika katika kijiji cha Kikokwe Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga.
Tangu kuingizwa kwa zao hili lilikua linalimwa na Makampuni makubwa na liliendeshwa na wakoloni ilipofika mwaka 1967 ambapo mwaka huo kulikua na sera ya utaifishaji asilimia (60%) ya mashamba yaliatifishwa na serikali na asilimia 40% yalibaki kuendeshwa na Kampuni binafsi.
Mwaka 1970 Serikali iliamua kuanzisha kilimo cha wakulima. wadogo Kabuku Wilayani Handeni Mkoani Tanga kikafeli sababu wakulima wakulima hao hawakuandaliwa kitaalam.
1980 Serikali ilitaka kuanzisha kilimo hicho eneo linaitwa Kimamba Wilaya ya Kilosa kikafeli kilishindwa kuendelea kwa sababu zilezile za Kabuku.
1999 kilimo hicho kilianzishwa tena Wilaya ya Korogwe mashamba.ya Hale ,Magunga ,Magona Mwelia na Ngombezi ambapo kilimo hicho kilionesha mafanikio na inaendelea hadi sasa.
Aidha amefafanua kwa kusema kuwa zao la Mkonge ni zao linalostahmili ukame , magonjwa na halina muda maalumu wa kupandwa na kuvunwa halina changamoto ya magonjwa wala wadudu.
Akizungumzia kuhusu idadi ya wakulima amesema imeongezeka na hali yao kiuchumi iko vizuri na zao la Mkonge limekua na bei nzuri.
Mwaka 2019 hadi 2020 kulikua na wakulima 7,000 huku katika kipindi cha 2025-26 idadi imeongezeka na kufikia wakulima zaidi ya 13 ,000 ,kilichochangia kuongezeka wakulima hawa ni baada ya kupata hamasa iliyofanywa na serikali pamoja na Bodi ya Mkonge iliyoambatana na elimu ya kilimo bora cha zao la Mkonge pamoja na uboreshaji wa usindikaji wa zao hilo umeongezeka na kuleta hamasa kubwa kwa wakulima wa Mkonge.
Amebainisha kuwa zao hili la Mkonge linalimwa na kumea katika mikoa 16 nchii ameitaja baadhi ya Mikoa hiyo kuwa ni Tanga Pwani, Morogoro, Kilimanjaro,
Arusha,Dodoma, Singida, Tabora, Mara ,Lindi Mtwara,Simiyu,Shinyanga, Kigoma,Geita,
Katavi ,Kagera na Ruvuma.
Kuhusu soko la Mkonge amesema kuwa asilimia 75% ya zao hilo linauzwa nje ya nchi huku asilimia 25%inauzwa soko landani huku akisisitiza kwamba soko la ndani siyo zuri sana sababu ya ushindani na bidhaa za Manila (Plastic).
Amesema kuwa hii ndiyo changamoto wanayokutana nayo kwa sababu bidhaa nyingi zinatengenezwa na Manila (Plastic) ikiwa ni katika matumizi mapya kama mifuko ya vifungashio zamani ilikua magunia ya unga mchele sukari, maharage na nyingine vilibebewa kwenye magunia ya katani tofauti na ilivyo sasa hata makapeti yamekua yakitengenezwa kwa kutumia Manila.
Amesema mwaka 1964 Tanzania ilikua ikiongoza kuzalisha tani 2,300 huku katika kipindi cha 1990 uzalishaji wa zao la Mkonge ulishuka na kufukia 23,000.





0 Comments