WIZARA YA HABARI , UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO YAFANYA MABADILIKO YA SERA

Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Maendeleo ya Michezo, inapenda kuwafahamisha wananchi kwamba imefanya mabadiliko ya Sera ya Michezo ya mwaka 1995 na sasa itatoa sera mpya ya mwaka 2016 ambayo wadau mbalimbali wameshiriki kwa kutoa maoni yao ili yatumike kuboresha Sera hii mpya.

Wizara kwa mara nyingine tena inategemea kupokea maoni kupitia Tovuti Rasmi ya wananchi ambayo ni www.wananchi.go.tz ambapo rasimu ya Sera hii mpya ya mwaka 2016 inapatikana katika tovuti ya wizara ambayo ni:www.habari.go.tz,na kwa wale wanaoweza kufika ofisini kwetu Golden Jubilee Towers ghorofa ya 8 au kupitia barua pepe ifuatayo, nicholaus bulamile@habari.go.tz.

Maoni hayo yatakuwa yamelenga katika maeneo makuu kumi ambayo ni; Kuwa na jamii inayoshiriki katika michezo na mazoezi ya viungo vya mwili kwa afya endelevu na msingi wa maendeleo ya michezo.

Kuwa na wataalamu wa michezo wanaokidhi viwango na mahitaji. Kuwa na mifumo anuai na thabiti ya uratibu, usimamizi na uendelezaji wa michezo.

Kuimarisha ajira na mikataba katika michezo. Kuwa na uwekezaji unaokidhi mahitaji ya maendeleo ya michezo.

Kuwa na tafiti endelevu katika michezo. Kuwa na mfumo thabiti wa utoaji huduma za bima, kinga, tiba na uthibiti wa matumizi ya dawa na mbinu haramu katika michezo.

Kuwa na maendeleo endelevu ya utalii wa michezo. kuwa na mfumo shirikishi wa utoaji wa habari za michezo.

Kuwa na utaratibu wa kumlinda mwanamichezo dhidi ya maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Wizara inapenda kutoa wito kwa wadau wote washiriki kutoa maoni yao yenye tija ambayo yataboresha Sera ya maendeleo ya Michezo ya mwaka 2016.

Ukusanyaji wa maoni utaanza leo tarehe 29 Februari hadi tarehe 5 Machi 2016.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,​ Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Post a Comment

0 Comments