WADAU wa muziki wa dansi watapata burudani ya aina
yake katika onyesho maalum ambalo
litawakutanisha pamoja bendi kongwe za muziki wa dansi za Twanga Pepeta na FM Academia.
Onyesho hilo ambalo limepangwa kufanyika Machi 28, kwenye viwanja vya Leaders Club
Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Itafahamika kwamba bendi hizi mbili ambazo kuna wakati
walikuwa mahasimu wakuu hali
iliyopelekea kuwa na upinzani wa hali ya juu.
Aidha wadau wamezibatiza jina na kuwaita Ukawa wa kudumu
ambapo watapanda jukwaani kwa mara ya kwanza
na kutumbuiza pamoja.
Hii ni kwa sababu
hizi ni bendi pekee za kizazi cha tatu cha muziki wa dansi nchini ambazo
zimedumu muda mrefu na zina washabiki wengi zaidi.
Hii ni sawa sawa na Msondo na Sikinde (bendi za kizazi cha pili cha muziki wa dansi nchini) walivyoanza mipambano mwaka 1991. Hivi sasa imekuwa kama Simba na Yanga kwa vile mpira ni tofauti na muziki, ilikuwa ni muhimu kuwa na aina nyingine ya mpambano wa kizazi kipya.
Akizungumza na
Jana Meneja wa bendi ya Twanga Pepeta Hassan Rehan alisema pambano hili ni moja ya njia ya kurudisha umaarufu wa
muziki wa dansi nchini.
Muziki wa Bongo Fleva una chachu kubwa ya tamasha la
Fiesta ambayo hukutanisha wanamuziki wengi pamoja hivyo muziki wa dansi ulikuwa hauna matukio
ya kuzikutanisha bendi tofauti
kiushindani ukiachia kwenye kusindikiza uzinduzi wa album mpekee.
Kwa upande wa FM Academia watakaopanda jukwaani ikiwa na
‘Dream Team’ kundi linaloundwa na Rais
wa bendi hiyo Nyoshi El Saadat , Patcho Mwamba, King Blaise, Pablo Masai, Levi
Boy, Totoo Kalala, Kalidjo, G-seven, Elombe Kisinja, Moses Ebonga Katumbi ‘Jesus’ ,Baratele Hatibu
na wengine wengi .
Huku bendi ya Twanga Pepeta ikiongozwa na Kiongozi wa
bendi Luizer Mbutu, Haji Ramadhani, Kalala Junior, Saleh Kupaza na wengine.
0 Comments