NA MIKA NDABA
MSAANI wa muziki wa Hip hop
nchini, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ jana amekiri kutumia dawa za kulevya katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kuomba asomewe mashtaka yake upya.
Awali kabla ya kusomewa
mashtaka yake, mbele ya Hakimu Mkazi, Warialwande Lema, wakili wa seikali
Diyana Lukondo alieleza kwamba kesi hiyo ipo kwa ajili ya kutajwa na kuomba
kupangiwa tarehe nyingine.
Baada ya kutoa maelezo hayo,
Chid benzi alinyoosha mkono na kuomba asomewe upya mashtaka yanayomkabili ili
aweze kuyajua.
Akimsomea upya mashtaka yake,
Wakili Lukondo alieleza kuwa msanii huyo, anakabiliwa na mashitaka matatu ya
kupatikana na dawa za kulevya aina ya Bangi na Heroin Hydrochloride na vifaa
vinavyotumika katika uvutaji wa dawa hizo.
Alieleza kwamba mnamo Oktoba
24, mwaka jana, Chid Benzi alikutwa na madawa hayo yenye thamani ya sh.40, 358
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Baada ya kusomewa mashtaka
hayo, Chid alikiri kuhusika na kitendo hicho.
Hakimu Lema aliahirisha
shauri hilo hadi Februari 23, mwaka huu, kwa ajili ya kusomewa mashtaka ya
awali(PH).
Hakimu Lema alisema kuwa
dhamana ya mshtakiwa huyo bado inaendelea.
0 Comments