MAGWIJI wa muziki wa dansi
nchini bendi za Mlimani Park Orchestra ‘Sikinde’ na Msondo
Ngoma Band
siku ya Iddi Mosi watachuana vikali katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Temeke.
Mpambano huo ambao utakwenda kwa jina la Nani Mtani Jembe ni kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Id El Fitr na pia litaamua ni bendi ipi kali kati yao.
Mratibu wa mchuano huo, Joseph Kapinga amesema pambano hilo litaanza saa nane alasiri hadi majogoo.
Kapinga alisema bendi zote mbili ziko msituni kujiandaa na mpambano huo.
Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kulinda upinzani wao.
Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera amesema watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaisambaratisha Sikinde.
Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede, Mabera, Eddo Sanga, Juma Katundu, Roman Mng’ande `Romario’ na Hassan Moshi.
Naye kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.
“Tuna waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.
Baadhi ya wanamuziki wanaounda Sikinde ni Hassan Rehani Bitchuka "Stereo", Hassan Kunyata, Abdala Hemba, Musemba Waminyugu.
Romario akiwa katika jukwaa la Msondo ngoma.

0 Comments