SUBIRA MGALU ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE.JIMBO LA BAGAMOYO ,PWANI


Bagamoyo, Juni 29, 2025

 – Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Jimbo la Bagamoyo, Mkoani Pwani, Mhe. Subira Khamis Mgalu, leo amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Bagamoyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mhe. Mgalu amepokea fomu hiyo katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Bagamoyo, ambapo alikabidhiwa rasmi na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Bagamoyo, Shabani Karage.

Hatua hiyo inaashiria nia ya dhati ya Mhe. Subira Mgalu kurejea katika nafasi ya uongozi wa moja kwa moja jimboni, ambapo anatarajiwa kushindana na wagombea wengine ndani ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Subira Mgalu ni miongoni mwa wanasiasa wanawake waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, na hatua yake ya kurejea katika kinyang'anyiro cha ubunge inatazamwa kama sehemu ya kuendeleza mchango wake katika maendeleo ya kisiasa na kijamii ndani ya Wilaya ya Bagamoyo.

 

Post a Comment

0 Comments