EXTRA BONGO KULA EID EL FITR KANDA YA ZIWA

MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo Ally Choki  pichani  juu ametoa ratiba ya maonesho ya bendi yao ambayo watatumbuza katika kusherehekea sikuku ya Eid el Fitri mwaka huu.Choki alisema katika onyesho lao la kwanza  watakuwa katika ukumbi wa Jembe Beach uliopo  jijini Mwanza , na Idd pili watakuwa mkoani Shinyanga huku Idd tatu wakatuwa Bariadi.Aliongeza kwa kusema kuwa Agosti mosi wanatarjia kufanya onyesho mkoani Musoma  wakati Agosti mbili watakuwa Wilayani Kahama na Agosti tatu watamalizia ziara yao  Geita.Wakiwa katika ziara hiyo mikoani bendi ya Extra Bongo watatumia fursa hiyo kuutangaza wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la ‘Kichwa Chini’  ambao waliuzindua siku chache kabla ya Mwezi  mtukufu wa Ramadhan.Bendi hiyo almaarufu kama ‘Wazee wa Kizigo’  ‘Regina Zanzibar’, ‘Mtenda akitendewa’ , ‘Neema’  na nyinginezo.Choki amewaahidi wakazi wa mikoa ya kanda ya Ziwa kujitayarisha kupata burudani ya aina yake.

Post a Comment

0 Comments