MISS UTALII TANZANIA, KUITANGAZIA DUNIA KUPATIKANA KWA NYATI WA AJABU NA PEKEE DUNIANI KATIKA HIFADHI NGORONGORO.



Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana kwa nyati mweupe wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro, imekuwa ni chachu na kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati wake wa kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo kwa kuanzia ameamua kuanza kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia anayokwenda kushiriki ya Miss Tourism World 2013, ambayo mwaka huu yanafanyikia nchini Equatorial Guinea Octoba 12, 2013.
Kupatikana kwa Nyati huyo wa ajabu Mweupe, ambaye hapatikani sehemu nyingine yoyote Duniani, wakati huu ambao anakwenda katika mashindano hayo ya Dunia, imekuwa ni fulsa ya pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwake , kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni Ajabu la Asili la Dunia Barani Afrika. Ambapo sasa Ngorongoro Crater  pamoja na maajabu ya bonde lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo wa Binadamu wa kale zaidi Duniani, Mchanga wa ajabu unao hama kila mwaka kwa umbo la Nusu mwezi, Mlima wenye Volkano Hai wa Oldonyo Lengai, lakini pia ushirikiano wa kuishi bila kudhuriana wa binadamu na Wanyama katika hifadhi hiyo na upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama wakubwa (BIG FIVE) na adimu duniani wakiwemo Faru Weusi,Duma,Mbwa Mwitu, Kaka kuona n.k.
 
Ngorongoro Crater na Hifadhi nzima ya Ngorongoro ni tunu ya Taifa la Tanzania, nahazina ya Dunia ambayo tunapaswa kuienzi na kuitangaza kwa nguvu zetu zote, ili iweze kuingiza pato na kuchangia zaidi uchumi na pato la Taifa, lakini pia kukuza na kuendeleza huduma za jamii ,ikiwemo elimu na afya. Naupongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa jitihada zao za kukuza utalii na kupambana na majangili , nawaomba kuimarisha na kuongeza mapambano na vita dhidi ya ujangili na majangili, ili kuhakikisha kuwa majangili hao hawamdhuru nyati huyo wa ajabu na Wanyama wengine katika hifadhi hiyo. Lakini pia naiomba mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kumlinda nyati huyo dhidi ya Wanyama wengine wala nyama kama samba n.k.
Wafanyakazi wa hifadhi hiyo Ijumaa ya tarehe 27-9-2013 asubuhi wakiwa katika basi la mamlaka wakienda kazini walimshudia Nyati huyo akiwa na kundi la nyati wengine kandokando ya barabara ndani ya hifadhi hiyo. Jambo ambalo liliwavutia na dereva wa basi hilo kulazimika kusimamisha basi kutoa fulsa kwa wafanyakazi hao kumshudia nyati huyo na baadhi yao kupiga picha kwa simu zao na kamera walizokuwa nazo.
Hadija ameushukuru uongozi wa Ngorongoro , kwa kumpatia DVD zaidi ya 100 ya hifadhi hiyo,ambazo atakwenda kuzigawa kwa washiriki wote 126 na vituo vya Televisheni vya nchi zao wanaoshiriki katika mashindano hayo ya Dunia ya Miss Tourism World 2013 mwaka huu. Baada ya kurudi nitazunguka nchi nzima na dunia nzima kuitangaza Ngorongoro kwa kushirikiana na Uongozi wa Miss Tourism Tanzania Organisation na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Post a Comment

0 Comments