Mshambuliaji wa timu ya Hazina, Seleman Juma (aliyeruka) akimiliki mpira mbele ya beki wa timu ya Ras Dodom, wakati wa mchezo wao wa ufunguzi wa mashindano ya SHIMIWI, uliochezwa jioni kwenye Uwanja wa Jamhuri. Katika mchezo huo timu ya Hazina imeibuka na ushindi wa mabao 3-1.
''Napita kushoto, we tulia tu......
Mtanange ukiendelea, ni Beki wa Hazina, Issa Ramadhan (wa nne kulia) akiambaa na mpira wakati wa mchezo huo.
Winga Tereza wa Hazina akichanja mbuga kujiandaa kumimina krosi...
Kipa wa Ras Dodoma, akiokoa moja ya hatari langoni kwake...
Timu zikijipanga kukaguliwa....kabla ya mtanange huo....
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala,
akisalimiana na wachezaji wa Hazina wakati akikagua timu hizo kabla ya
kuanza kwa mtanange huo.
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala,
akisalimiana na wachezaji wa Ras Dodoma, wakati akikagua timu hizo kabla
ya kuanza kwa mtanange huo.
Katika
mchezo wa Netiboli, ilikuwa ni patashika baina ya timu ya Tamisemi na
Bunge, ambapo hadi tunakwenda mitamboni Tamisemi walikuwa wakiongoza kwa
mabao mengi kwa machache...
Kipute cha netiboli, Tamisemi na Bunge kikiendelea.....
Huyu Centa wa TAMISEMI (mwenye mpira) we acha tu.....
Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia kipute cha netiboli....
Huku
nako katika mchezo wa Kamba, ilikuwa ni patashika kati ya timu za
wanawake za Hazina na Ikulu, ambapo kwa upande wa wanawake, timu ya
Hazina imeweza kuwagalagaza Ikulu, lakini katika picha hizi angalia kama
sheria za mchezo huu zinaruhusu triki hii waliyoitumia kina mama hawa
ya kukaa chini bila kufanya chochote hadi dakika zilipomalizika na
kuibuka na ushindi huo.
Hawa
ndiyo Kina Mama wa Ikulu, wakionyesha juhudi zao za sifa ya 'Jiko',
lakini haikuwa bahati yao siku ya leo ambapo waliweza kukubali bila
kushurutishwa.
Hao bwana kwa kukaa hao weeeeee.........
0 Comments