Wasanii
wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma Mwana FA na Linah, wakiimba
kwa pamoja jukwaani, wakati wa shoo yake ya 'The Finest' iliyofanyika
kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana usiku.
Katika onyesho hilo lilihudhuliwa na baadhi ya Viongozi wa vyama vya
Siasa pamoja na wasomi kibao kutoka Vyuo mbalimbali. Miongoni mwa
wanasiasa walioonekana kwa haraka haraka ukumbini hapo ni pamoja na
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, aliyeketi na kuparty pamoja na
Mbune wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
********************************
Halima Kambi, Dar
KATIKA
Shoo hiyo ya 'Kijanja' pia ilihudhuliwa na wasomi kibao huku baadhi ya
wabunge kama Zitto Kabwe na January Makamba wakiwa ni miongoni mwa
mashabiki wajanja waliohudhuria katika shoo hiyo ya "kijanja" ya The
Finest Kama Zamani iliyofanyika katika Ukumbi Makumbusho ya Taifa Dar
es Salaam, jana usiku.
Mwana
FA, pia alisindikizwa na na baadhi ya wasanii kama, Ben Paul, Linah,
Maua, Dully Sykes na wengine kibao pamoja na bendi ya Njenje
Kiukweli
show ilifana sana kutokana na utaratibu na mpangilio na maandalizi ya
shoo yenyewe na MwanaFA aliweza kufanya yake jukwaani na kuwapagawisha
mashabiki wake katika usiku ule.
Kutoka
(kulia) ni Mbune wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akiwa na Mbunge wa
Bumbuli (CCM) January Makamba, wakiwa ni miongoni mwa mashabiki wa Mwana
FA, waliohudhulia shoo hiyo. Kushoto ni Mtangazaji wa Clouds FM, Gerald
Hando.
Mwana FA, akishambulia jukwaa kwa mistari ya kina.....
Sehemu ya warembo mashabiki wa Mwana FA, wakijitahidi kunasa matukio kupitia simu zao za mkononi.
0 Comments