NMB YASHIRIKI MAONYESHO BUNGENI



Waziri wa Nchi ya Ofisi ya Waziri mkuu (Sera,Utaratibu na Bunge)William Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa ofisa wa benki ya NMB  Diana Kimaro mara alipotembelea banda la NMB katika maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge.
Mbunge wa viti maalum, Mh. Zainabu Vulu akipata maelezo kutoka kwa Meneja Huduma za Ziada, Alluthe Nungu wakati walipotembelea banda la NMB.
Baadhi ya maofisa wa benki ya NMB waliopo kwenye maonyesho ya taasisi za kifedha mjini Dodoma.
Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa mbunge wa viti maalum, Mathew Mlacha na Mbunge wa Busega, Titus Kamani  juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na benki ya  NMB.
Na Mwandishi Wetu
Benki ya NMB inashiriki maonyesho ya huduma za kibenki yanayoendelea katika viwanja vya Bunge mkoani Dodoma. Lengo la maonyesho hayo ni kuelezea huduma mbali mbali zitolewazo na benki ya NMB kwa wateja wake.

Post a Comment

0 Comments