KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAAHIDI KUENDELEZA UDHAMINI TAMASHA LA BULABO.



12. Kikundi cha ngoma cha basesilia BujoraKikundi cha ngoma cha Basesilia Bujora, kikionyesha umahiri wake ambapo waliibuka washindi wa siku ya mwisho ya tamasha la Bujora ambapo walishinda na kuibuka na kitita cha shilingi laki mbili na thelathini baada ya mpinzani wao upande wa pili kutoka Musoma kuingia mitini, Tamasha hilo lilidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.2. Mshindi wa siku ya kufunga tamasha_Basesilisa BujoraKiongozi wa kikundi cha Basesilia Bujora, akionyesha umahiri wake wa kucheza na nyoka katika siku ya mwisho wa tamasha hilo ambapo kikundi chake kiliibuka washindi wa siku hiyo, Tamasha hilo lililodumu kwa takribani wiki nzima lilivutia maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza  lilidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager. 6. Mkuu wa Wilaya ya MaguMkuu wa wilaya ya Magu Ndugu  Jacquiline Liana akizungumza na wananchi katika tamasha hilo. 7. Umati uliofurika kuangalia siku ya kufunga sherehe za BulaboUmati wa wakazi wa Wilaya ya Magu wakifuatilia kwa makini ngoma za jadi kutoka kabila la wasukuma ‘Bulabo’ katika kiwanja cha Kisesa. Tamasha hilo lililodumu kwa takribani wiki nzima lilivutia maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza  lilidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.
8. Kikundi cha Ngoma cha Basesilia BujoraWapiga ngoma za asili wakipiga ngoma 9. Kikundi cha Basesilia Bujora kaziniKwa shangwe kubwa maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Magu jijini Mwanza wamekuwa wakishuhudia burudani ya ngoma za asili za kabila la wasukuma ’Bulabo’ ambalo limemalizika siku ya Jumapili jioni katika uwanja wa Kisesa jijini Mwanza. Katika sherehe hizo za kiutamaduni vikundi ishirini na nane kutoka makabila ya wasukuma  vilishiriki na kuzifanya sherehe hizo zivutie zaidi. Kampuni ya bia ya Serengeti imeahidi kuendelea kudhamini tamasha la ngoma za kabila la wasukuma ’Bulabo’ ambazo ni maalum kwa ajili ya kusheherekea sikukuu za mavuno kila mwaka. 
“Tunayofuraha kubwa kwa mara nyingine tena kuona tumeweza kuungana na wenzetu wa kabila la wasukuma katika kipindi cha wiki moja sasa na kusherehekea furaha yao baada ya mavuno huku wakiendelea kuzienzi tamaduni zao. Ni kwa mara ya nane sasa tumekuwa tukidhamini sherehe hizi za bulabo na tunaahidi kuendelea kudhamini kwani sherehe hizi zina mchango mkubwa kwa wasukuma na taifa kwa ujumla”. Alisema jaji Mark Bomani mwenyekiti wa kampuni ya bia ya serengeti. 
Kampuni ya bia ya Serengeti imekuwa ikidhamini tamasha hilo kwa takribani mwaka wa nane sasa,ambapo waandaaji wameishukuru kampuni hiyo kwa kuwezesha na kufanikisha tamasha hilo, ”Napenda kutoa shukrani zetu kwa kampuni ya bia ya Serengeti ambayo imekuwa mdhamini wetu kwa muda mrefu sasa inafika miaka minane, tumekuwa nao bega kwa bega na hasa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo Mheshimiwa Mark Bomani ambae pia ni mlezi wetu hapa Bujora” alisema Padri Mhoja, muandaaji wa tamasha hilo.
Naye mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Jacquieline Liana, ameipongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kudhamini tamasha hilo na kuomba wadau wengine kujitokeza kudhamini kama wenzao wa kampuni ya bia ya Serengeti wanavyofanya, pia aliwaasa vijana kuacha tabia za kunywa pombe wakati wa kazi na badala yake wafanye kazi kwa bidii ili waje kusheherekea sherehe hizi za Bulabo mwakani.
Katika sherehe hizo za Bulabo vikundi vilivyoshiriki vilishindana kwa mtindo wa mtoano ambapo vikundi viwili vikiwa katika pande mbili tofauti za uwanja vikitenganishwa na bendera nyekundu, huku majaji wakiangalia ni kundi lipi lenye umati mkubwa hivyo ni kuashiria kuwa mwenye watu wengi zaidi ndiye mwenye mvuto zaidi na hapo kutangazwa mshindi. Kigezo kingine kichokuwa kikiwafanya washiriki waongeze jitihada katika kucheza na kujikuta wakiwapa raha zaidi watazamaji ni kile cha kundi linaloshindwa kutakiwa kutoa elfu thelathini katika laki mbili ambazo zilikuwa zikitolewa kwa kila kundi na kumpa mshindi. 
Washindi katika ngoma hizo zilizodumu kwa takribani wiki moja ni Nghomi Lukala, Kanigini Hindiya, Kibola Shitungulu, Bagehu Lukala, Mayokagose, Kinasa Ncheye, Nyamuitabungagwa Mnkoti, Mabeshi Lukwaja, Nyeyewaza, Shigulu Dema, Bulolo Shokolo, Seleleko na Basesilia Bujora aliyemalizia siku ya Jumapili baada ya mpinzani wake kuingia mitini.

Post a Comment

0 Comments