Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, akiwakatika mazungumzo na Mjumbe wa Tume ya Uongozi
wa Taifa wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Liu Yunshan, kwenye
Ofisi za chama hicho mjini Beijing China. (Picha naBashir Nkoromo)
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwakatika mazungumzo na Mjumbe wa
Tume ya Uongozi wa Taifa wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Liu
Yunshan, kwenye Ofisi za chama hicho mjini Beijing China. Kushoto ni
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
NA BASHIR NKOROMO, BEIJING, CHINA
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema
Tanzania kuna wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi, lakini Chama
Cha Mapinduzi kinaamini kwamba wawekezaji walio wakubwa zaidi kwa tija
ni wakulima.
Kinana alisema hayo Machi 20, 2013, wakati akizungumza na Mjumbe wa Tume
ya Uongozi wa Taifa wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Liu
Yunshan, mjini hapa, akiwa katika ziara ya kimafunzo nchini China,
ambayo anafanya kwa mwaliko wa chama cha CPC, na amefuatana ujumbe wa
watu 14 wakiwemo viongozi waandamizi na maofisa wa CCM.
Kinana alisema, kutokana na kutambua mchango mkubwa katika kuweza kuinua
uchumi wa Tanzania, serikali ya Chama Cha Mapinduzi, imeanzisha na
kuusimamaia mpango wa Kilimo Kwanza kwa lengo la kuwezesha wakulima
walio wengi kuchangia uchumi wa taifa kupitia uwekezaji katika sekta
hiyo na hiyo pia kuinua hali za vipato vyao.
Alisema, ili kupata mafanikio zaidi na ya haraka, Serikali ya Chama Cha
Mapinduzi itautumia uzoefu wa jinsi Chama Cha Kikomunisti cha
kilivyoweza kuratibu na kusimamia kwa hali ya juu miradi ya kilimo hadi
kuiwezesha China kuinuka kiuchumi njia kuu ikiwa ni kupitia sekta ya
kilimomo.
Kinana alisema, alimwambia Liu, kwamba, Chama Cha Mapinduzi kinaona
umuhimu wa kuiga uzoefu wa China katika kukuza uchumi kwa kuwa misingi
ya kisiasa na na sera za Tanzania na nchi hiyo katika uchumi zinafanana
kwa kuwa zinalenga zaidi kunua hali za wanyonge ambao ni wajasiramali
wadogo wadogo katika uwekezaji kwenye shughuli mbalimbali na kilimo.
Alisema, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, kinakaribisha mataifa ya nje
ikiwemo China kushiriki katika uwekezaji, lakini akabainisha kwamba
uwekezaji ambao Tanzania inahitaji zaidi ni ule utakaonufaisha pande
zote, Tanzania na nchi itakayohusika na kwamba baadhi ya faida ambazo
inatarajia Tanzania kuzipata ni uwekezaji ambao utatengeneza nafasi
nyingi za ajira kwa Watanzania.
Kuhusu siasa za nje, Kinana aalimwambia Liu kuwa, Chama Cha Mapinduzi
kinasisitiza kama chama tawala, kwa kwamba Tanzania ni nchi huru hivyo
haichaguliwi rafiki bali yenyewe ndiyo inayochagua kulingana na faida
ambayo Watanzania wataipata, na haitafuata msukumo au mapendekezo ya
taifa lolote la nje na kusisitiza kwamba Tanzania na China zina urafiki
wa kihistoria tangu wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za kusini
mwa Afrika.
"Na tutaendelea kuundumisha urafiki huu wa kindungu ulioanzishwa na
waasisi wa mataifa yetu, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa upande wa
Tanzania na hayati Mao Tsetung kwa upande wa China", alisema Kinana na
kuongeza;
"Tunaamini Tanzania inayo mengi ya kujifunza kutoka China kama ilivyo
China nayo kuwa na mengi ya kujifunza kutoka Tanzania, tunaamini ziara
ya Rais wa China Xi Jinping nchini Tanzania, itakayoanza (Jumamosi),
mara baada tu ya kuchaguliwa rasmi kuwa rais wa nchi yake, ni alama
muhimu ya namna chama cha kiongozi huyo ambacho yeye ni Katibu Mkuu,
kinavyothamini uhusiano wake na CCM na Watanzania kwa jumla.
Alisema, kauli aliyotoa Rais Ping katiba Bunge Kuu la China,
inayosisitiza nchi hiyo kuendelea kupambana na umasikiniu, kuondoa
urasimu na umangimeza, kuimua hali za wananchi na kudumisha amani
duniani inastahili kupongezwa na kila mpenda maendeleo duniani kote.
Kwa upande wake, Liu katika mazungumzo hayo, aliipongeza CCM kwa namna
inavyoongoza, uongozi ambao amesema kutokana na umadhubuti umeweza
kuifanya Tanzania kupiga hatua ya kubwa kiuchumi na kisiasa ambapo nchi
imeendelea kuwa ya amani na utulivu na kuahidi CPC kuendeleza na
kuimarisha uhusiano na CCM kwa manufaa ya serikali ya Tanzania na
wananchi kwa jumla.
Alisema Tanzania chini uongozi wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete, imeweza kupiga hatua kubwa ingawa bado zipo changangamoto
nyingi za kushughulikiwa na kueleza imani yake kwamba chini ya Rais
Kikwete Tanzania itanedelea kuwa Umoja, amani na mshikamano vitasaidia
kuleta maendeleo zaidi Tanzania.
Kiongozi huyo aliasa kuwa upo umuhimu wa kuimarushwa Chama Cha Mapinduzi
ili kiendelee kupambana na uninafsi, kujenga uaminifu na kutumikia
wananchi kwa kufuata misingi mikuu ya uongozi bora. " pia nakupongeza
mheshimiwa Kinana kwa kuteuliwa kuwa katibu Mkuu wa Chama, naamini
kuteuliwa kwako kumezingatia mchango mkubwa uliokwishatoa kwa taifa la
Tanzania na uchapakazi wako.
0 Comments