ASKOFU MKUU JIMBO KUU KATOLIKI LA DAR ES SALAAM AWAHIMIZA WAKRISTO KUDAI HAKI

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi, amewahimiza Wakristo kuwa wadau wa haki akisisitiza kuwa “hakuna amani ya kudumu bila haki.”

Akihubiri wakati wa mkesha wa Krismasi, Askofu Ruwa’ichi alisema, “Sisi sote kwa nguvu ya ubatizo wetu tunaitwa tuwe watu wa haki… haki ni kutambua mastahili ya wengine na kuyaheshimu.”

Amewakumbusha waumini kujitathmini kwa kuuliza, “Ewe mwana wa Dar es Salaam, ewe Mtanzania, je wewe ni mtu wa haki?”

Post a Comment

0 Comments